Pata taarifa kuu

Zoezi la kuondolewa kwa wageni kutoka Gaza kwenda Misri lasitishwa, Hamas yatangaza

Serikali ya Hamas imesitisha zoezi la kuwaondoa wageni na raia wenye uraia pacha kutoka Gaza kwenda Misri, kutokana na Israel kukataa kuwaruhusu Wapalestina waliojeruhiwa kuondoka kwenda hospitali za Misri, afisa wa Hamas ameliambia shirika la habari la AFP siku ya Jumamosi, Novemba 4.

Kivuko cha Rafah kati ya Israel na Misri, hapa ilikuwa tarehe 1 Novemba 2023.
Kivuko cha Rafah kati ya Israel na Misri, hapa ilikuwa tarehe 1 Novemba 2023. REUTERS - STAFF
Matangazo ya kibiashara

"Hakuna mwenye hati ya kusafiria ya kigeni atakayeweza kuondoka katika Ukanda wa Gaza kabla ya majeruhi ambao wanatakiwa kuondoka kutoka hospitali za kaskazini mwa Ukanda wa Gaza kusafirishwa hadi kwenye kivuko cha Rafah", kivuko kati ya Palestina na Misri, afisa huyo amesema kwa masharti ya kutotajwa jina.

Wakati huo huo Mkuu wa Majeshi wa Israel Jenerali Herzi Halevi amesafiri kwenda Ukanda wa Gaza siku ya Jumamosi kwa ajili ya kuwatembelea wanajeshi wake, ikiwa ni mara ya kwanza tangu kuanza kwa vita dhidi ya Hamas iliyo madarakani katika ardhi ndogo ya Palestina. "Ndiyo, alikuwa katika Ukanda wa Gaza leo," msemaji wa jeshi ameliambia shirika la habari la AFP, baada ya picha kurushwa kwenye televisheni ya serikali ya Israel.

Yoav Gallant, Waziri wa Ulinzi wa Israeli, amehakikisha kwamba nchi yake "itampata" kiongozi wa Hamas huko Gaza na "kumuangamiza".

► Akiwa zirani nchini Jordan, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken amekariri kwamba Israel ina haki ya kujilinda a kujihami, lakini pia amekumbusha msimamo wa Marekani wa kuunga mkono "kusitishwa wa mapigano kwa minajili ya kutoa misaada ya kibinadamu" kwa raia wa Gaza.

► Tangu Oktoba 7, zaidi ya Waisraeli 1,400 wameuawa, wakiwemo wanajeshi 341, na jeshi la Israel linaripoti watu 240 wanaoshikiliwa mateka na Hamas. Wizara ya Afya ya Hamas ilmeangaza mnamo Novemba 4 idadi ya vifo vya Wapalestina 9,488, wakiwemo watoto 3,900.

► Wizara ya Afya ya serikali ya Hamas ilitangaza kuwa watu 12 wameuawa katika shambulio la bomu la Israel lililopiga shule ya Umoja wa Mataifa ambapo watu waliokimbia makazi wanapewa hifadhi, katika kambi ya wakimbizi katika Ukanda wa Gaza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.