Pata taarifa kuu

Antony Blinken anazuru Jordan kutafuta suluhu ya mzozo wa mashairiki ya kati

Nairob – Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Antony Blinken, ameanza vikao na mawaziri wa mambo ya nje kutoka katika mataifa ya kiarabu huko Jordan, ikiwa ni njia moja ya kujaribu kumaliza vita vya Gaza vilivyodumu kwa takriban mwezi mmoja.

Hii ni ziara ya pili ya mwanadiplomasia huyo mkuu wa Marekani mashariki ya kati kujaribu kupata suluhu ya vita vya Gaza
Hii ni ziara ya pili ya mwanadiplomasia huyo mkuu wa Marekani mashariki ya kati kujaribu kupata suluhu ya vita vya Gaza AP - Jonathan Ernst
Matangazo ya kibiashara

Haya yanajiri wakati huu wanajeshi wa Israel wakiwa wameuzingira mji mkubwa zaidi wa Gaza, kwa kile wanachosema ni kujaribu kuangamiza na kumaliza kundi la wapiganaji wa Hamas  na kulipiza kisasi kwa shambulio la Oktoba 7 ambalo maafisa wa Israel wanasema liliua takriban watu 1,400 katika ardhi ya Israel, wengi wao wakiwa raia.

Wizara ya afya huko Gaza, inayoendeshwa na Hamas, inasema zaidi ya raia 9,200 wa Gaza  wengi wao wakiwa wanawake na watoto wameuawa katika mashambulio ya  Israel.

Shule hiyo ilikuwa inatoa hifadhi kwa wakimbizi katika ukanda wa Gaza
Shule hiyo ilikuwa inatoa hifadhi kwa wakimbizi katika ukanda wa Gaza REUTERS - ANAS AL-SHAREEF

Hamas imesema shambulio la Israel kwenye shule inayoendeshwa na Umoja wa Mataifa katika ukanda wa Gaza ambapo wakimbizi walikuwa wanapata hifadhi limesababisha vifo vya watu 20.

Jeshi la Israel linasema mji wa Gaza ni kitovu cha kundi la kigaidi la Hamas likisema kuwa mashambulio yake yanawalenga wapiganaji wa kundi hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.