Pata taarifa kuu

Jeshi la Israeli limeendelea kutekeleza mashambulio katika ukanda wa Gaza

Nairobi – Jeshi la Israeli, limeendelea kutekeleza mashambulio katika eneo la Gaza, likilenga shule, hospitali, magari ya wagonjwa na makaazi ya watu, katika kile inachosema inaendelea kuwasaka wapiganaji wa kundi la Hamas.

Mashambulio ya leo, yamesababisha vifo vya watu, 15 katika shule ya Al-Fakhoura iliyo kwenye  kambi ya wakimbizi ya Jabalia
Mashambulio ya leo, yamesababisha vifo vya watu, 15 katika shule ya Al-Fakhoura iliyo kwenye  kambi ya wakimbizi ya Jabalia REUTERS - ANAS AL-SHAREEF
Matangazo ya kibiashara

Mashambulio ya leo, yamesababisha vifo vya watu, 15 katika shule ya Al-Fakhoura iliyo kwenye  kambi ya wakimbizi ya Jabalia.

Jeshi la Israeli inasema inatekeleza mashambulio hayo, kwa sababu yanatumiwa na kundi la Hamas, na wapiganaji wake wanajicha katika miundo mbinu hiyo.

Hatua ya Israeli kushambulia msafara wa magari ya wagonjwa katika ukanda wa Gaza imekashifiwa na katibu mkuu wa UN
Hatua ya Israeli kushambulia msafara wa magari ya wagonjwa katika ukanda wa Gaza imekashifiwa na katibu mkuu wa UN AFP - MOMEN AL-HALABI

Katika hatua nyingine, Mawaziri wa Mambo ya nje kutoka nchi za Kiarabu na mwenzao kutoka Marekani Anthony Blinken, wanakutana nchini Jordan kujadili mzozo huo, wakati huu kukiwa na shinikizo kwa Israeli kusitisha mashambulio ili kuwasaidia, wakaazi wa Gaza.

Mawaziri wa Mambo ya nje kutoka nchi za Kiarabu na mwenzao kutoka Marekani Anthony Blinken, wanakutana nchini Jordan kujadili mzozo huo
Mawaziri wa Mambo ya nje kutoka nchi za Kiarabu na mwenzao kutoka Marekani Anthony Blinken, wanakutana nchini Jordan kujadili mzozo huo AP - Jonathan Ernst

Naye mjumbe maalum wa Marekani kwenye eneo la Mashariki ya Kati, anayehusika na masuala ya kibinadamu amesema, watu kati ya 800,000 hadi Milioni 1 wamekimbilia Kusini mwa Gaza, huku wengine karibu 400,000 wakisalia eneo la Kaskazini.

Tangu kuzuka kwa vita kati ya Israeli na Hamas, katika ukanda wa Gaza na kusabisha vifo vya Wapalestina zaidi ya Elfu 9 na watu wengine zaidi ya 1400 nchini Israeli wakiwemo raia 39 wa Ufaransa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.