Pata taarifa kuu

Israel yaghadhibishwa na hatua ya Australia yakubatilisha utambuzi wa Jerusalem

Mnamo 2018, Australia ilitambua Jerusalem Magharibi kama mji mkuu wa Israeli. Canberra imebadilisha uamuzi huu, uliochukuliwa wakati huo na Waziri Mkuu wa zamani kutoka chama cha Conservative Scott Morrison. Chama cha Labour, ambacho sasa kinatawala nchini Australia, kinaamini kwamba suala la hadhi ya Jerusalem "lazima litatuliwe ndani ya mfumo wa mazungumzo ya amani, kati ya Israel na watu wa Palestina, na sio upande mmoja".

Bendera ya Israeli inapepea katika mji wa Jerusalem nchini Israel.
Bendera ya Israeli inapepea katika mji wa Jerusalem nchini Israel. © Nick Brundle Photography / GettyImage
Matangazo ya kibiashara

Waziri Mkuu wa Israel Yaïr Lapid amelaani hatua hiyo ya Australia. Anashutumu mamlaka ya Australia kwa kuchukua uamuzi wa "haraka" katika kujibu habari "potofu" ya vyombo vya habari. 

Yair Lapid, pia ameongeza: "Tunaweza tu kutamani serikali ya Australia ishughulikie faili zake nyingine kwa umakini zaidi na kitaalamu". 

Katika taarifa, Lapid amesema kuwa Yerusalemu ni mji mkuu wa milele wa Israeli usiogawanyika na hakuna chochote kitakachobadilisha hilo.Katika mchakato huo, balozi wa Australia nchini Israel ameitishwa aweze kujieleza.

Mamlaka ya Palestina, kwa upande wake, imekaribisha uamuzi huo wa Australia na uthibitisho wake kwamba mustakabali wa uhuru wa Jerusalemu unategemea suluhisho la kudumu kulingana na uhalali wa kimataifa, amesema Hussein Al-Sheikh, afisa wa ngazi ya juu wa mamlaka ya Palestina. 

Haya ndiyo maafikiano yanayotetewa na jumuiya ya kimataifa. Kwa sababu chochote serikali ya Kiyahudi isemayo, Jerusalemu ya Mashariki imekaliwa vyema na kutwaliwa kinyume cha sheria. Kufanya Jerusalemu kuwa mji mkuu pekee na usiogawanyika wa Israeli ni kukiuka uhalali wa kimataifa.

Uamuzi wa serikali ya zamani ya Australia kutambua Jerusalem Magharibi kama mji mkuu wa Israel mwaka 2018 ulikuja baada ya Rais wa wakati huo wa Marekani Donald Trump kuchukua hatua kama hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.