Pata taarifa kuu

Mpalestina 1 auawa na 16 wajeruhiwa katika Ukingo wa Magharibi

Mpalestina mmoja ameuawa na wengine 16 kujeruhiwa wakati wa operesheni ya jeshi la Israel mapema Jumanne (Septemba 6) huko Jenin, katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu.

Wanajeshi wa Israel wakishika doria Machi 30, 2022 katika kijiji kilicho kusini mwa Jenin katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu, ambapo mshambuliaji mmoja wa Kipalestina anaaminika kukimbilia kabla ya kuwaua watu watano katika shambulio la awali la bunduki nchini Israel.
Wanajeshi wa Israel wakishika doria Machi 30, 2022 katika kijiji kilicho kusini mwa Jenin katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu, ambapo mshambuliaji mmoja wa Kipalestina anaaminika kukimbilia kabla ya kuwaua watu watano katika shambulio la awali la bunduki nchini Israel. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Operesheni ambayo imelenga kuharibu makazi ya mhusika wa shambulio baya la hivi karibni huko Tel Aviv, imetangaza Wizara ya Afya ya Palestina, ikinukuliwa na shirika la habari la AFP.

"Mhanga mmoja mwenye umri wa miaka 29 na watu 16 wamejeruhiwa kwa risasi au milipuko kutokana na uvamizi wa Israel dhidi ya Jenin," wizara ya Palestina imesema katika ujumbe mfupi kwa vyombo vya habari. 

Wakati wa usiku, jeshi la Israeli lilibaini kwamba lilifanya operesheni huko Jenin ili kuharibu makazi ya mhusika wa shambulio ambalo liliua watu watatu mnamo Aprili 7 katikati mwa mji wa Tel Aviv.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.