Pata taarifa kuu

Gaza: Hamas yawanyonga Wapalestina watano, wawili kati yao kwa 'ushirikiano'

Hii ni mara ya kwanza kutokea kwa takriban miaka mitano. Hamas, vuguvugu la Kiislamu lenye silaha, madarakani katika Ukanda wa Gaza tangu mwaka 2007, limewanyonga Wapalestina watano Jumapili hii asubuhi, Septemba 4, wakiwemo wawili kwa "kushirikiana" na Israel. Wengine watatu walipatikana na hatia kwa sababu ya "kesi za uhalifu," Hamas imesema katika taarifa, ikisema wafungwa wote "walipata haki yao kamili ya kujitetea" mbele ya mahakama.

Vijana wa Hamas wanajiandikisha katika kambi ya majira ya joto huko Khan Younis kusini mwa Ukanda wa Gaza, Agosti 18, 2017.
Vijana wa Hamas wanajiandikisha katika kambi ya majira ya joto huko Khan Younis kusini mwa Ukanda wa Gaza, Agosti 18, 2017. REUTERS/Mohammed Salem
Matangazo ya kibiashara

Wizara ya mambo ya ndani ya Ukanda wa Gaza imetoa maelezo machache kuhusu watu hao watano waliohukumiwa kifo. Walitambuliwa tu kwa herufi zao za kwanza au mwaka wao na tarehe ya kuzaliwa. Wawili kati yao waliuawa kwa kushirikiana na Israeli.

Mkubwa zaidi, aliyezaliwa mwaka 1968, amenyongwa asubuhi ya leo kwa kuipatia Israel habari tangu mwaka 1991 kuhusu wapiganaji wa Kipalestina na pia eneo la kutengeneza na kurusha roketi. Mwingine alipigwa risasi kwa kutoa taarifa kutoka 2001 ambayo inadaiwa ilisababisha "kuuawa shahidi" kwa raia wa Palestina.

Kwa mara ya kwanza tangu 2017

Watu wengine watatu waliouawa walikuwa wamehukumiwa kifo kwa mauaji, wizara hiyo inasema. Unyongaji wa mwisho unaojulikana huko Gaza ulitokea mwaka 2017. Katika miaka ya hivi karibuni, mamlaka huko Gaza imewahukumu vifo watu kadhaa kwa uhalifu mbalimbali au "kushirikiana" na Israeli, lakini hukumu hizi hazijatekelezwa.

Hamas imehalalisha mauaji haya kwa msingi wa Kanuni ya Mapinduzi ya Jumuiya ya Ukombozi wa Palestina, ambayo sio mwanachama.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.