Pata taarifa kuu

Israel: Jeshi latambua wajibu wake "unaowezekana" katika kifo cha Shireen Abu Akleh

Jeshi la Israel linakiri kuhusika katika kifo cha mwandishi wa habari wa Palestina Shireen Abu Akleh. "Kuna uwezekano mkubwa kwamba mwanajeshi wa Israel alimuua kwa bahati mbaya Shireen Abu Akleh," jeshi limesema. Mwandishi huyo nyota wa Al Jazeera aliuawa mwezi Mei mwaka huu wakati wa operesheni ya jeshi la Israel katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu. Jeshi hilo limetoa Septemba 5 ripoti ya uchunguzi wa kina kuhusu mazingira ya kifo chake.

Jeshi la Israel linakiri kuhusika kwane katika kifo cha mwandishi wa habari kutoka Palestina Shireen Abu Akleh mnamo Mei 11, 2022.
Jeshi la Israel linakiri kuhusika kwane katika kifo cha mwandishi wa habari kutoka Palestina Shireen Abu Akleh mnamo Mei 11, 2022. AP
Matangazo ya kibiashara

Ilichukua karibu miezi minne ya uchunguzi kwa jeshi la Israeli kutambua "kuhusika" kwake katika mauaji haya. Pia jeshi linaibua maana ya "uwezekano" wa mmoja wa askari wake na kutaja kwamba "haiwezekani kuamua kwa uhakika sababu za tukio hilo".

Mazingira ya tukio hilo, toleo la Israeli, ni kama ifuatavyo: asubuhi ya Mei 11, askari wa Israeli walifanya operesheni huko Jenin, kaskazini mwa Ukingo wa Magharibi unaokaliwa. Wanajeshi wa Israeli walikuwa katika eneo la mijini, ambapo walikuwa wakirushiana risasi na adui, pamoja na makundi ya wapiganaji wa Palestina.

Jeshi liliamua kuendelea na operesheni zake

Wakati wa operesheni, wanajeshi wa Israeli walifyatua risasi takriban mara ishirini. Risasi lililompata Shireen Abu Akleh lilipigwa "wakati wa mapigano [...] Huenda kulikuwa na hitilafu katika kutambua [mlengwa]", linaeleza jeshi.

Jeshi linasema "linasikitishwa" na kifo cha Shireen Abu Akleh, lakini linabaini kwamba limedhamiria kuendelea na operesheni zake za kupambana na "ugaidi"; neno linalotumika kuelezea upinzani wa kijeshi wa Palestina.

Familia ya mwanahabari huyo inadai waliohusika kuhukumiwa mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu na Marekani ijihusishe zaidi na kesi hii kwani mwandishi huyo aliyeuawa pia alikuwa raia wa Marekani.

Lina Abu Akleh, mpwa wa Shireen Abu Akleh, ametoa ushahidi kwenye alipokuwa akihojiwa na mwandishi wetu Sami Boukhelifa.

Haijalishi Waisraeli wanasema nini, tayari tunajua ukweli. Hatuwahitaji kuthibitisha kuhusika kwao. Tayari tunajua hilo. Kutoka mwanzo, kila kitu kimekuwa wazi katika kesi hii. Tunachotaka ni wale waliohusika na kifo cha Shireen kujibu uhalifu wao.

Lakini sio wauaji wa Shireen ambao watamtendea haki. Hatutarajii chochote kutoka kwa Waisraeli. Tunataka Umoja wa Mataifa na hasa Marekani kuchukua hatua.

Ikiwa Waisraeli watakubali wajibu wao katika kifo cha Shireen, basi watalazimika kujibu mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu. ICC lazima ifungue uchunguzi.

Nchini Israeli, hakuna kesi itakayofanyika na askari "pengine" hatahukumiwa, jeshi limesema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.