Pata taarifa kuu

Jordan: Mjadala wa bunge kuhusu usawa wa kijinsia wakatizwa na purukushani

Nchini Jordan, kikao cha bunge kililazimika kukatizwa siku ya Jumanne. Wajumbe walijadili suala kuhusu usawa wa kijinsia, wakaanza kupigana.

Amman, mji mkuu wa Jordan.
Amman, mji mkuu wa Jordan. Getty Images/Valery Sharifulin/Contributeur
Matangazo ya kibiashara

Je, neno la wanawake wa Jordan liongezwe kwenye sura yenye kichwa habari "haki na wajibu wa Wajordani"? Hili linaonekana kuwa swali ambalo limeibua mjadala katika muktadha wa mageuzi ya katiba yanayotafutwa na serikali. Kulingana na runinga ya serikali, wabunge kadhaa walipinga marekebisho haya ambayo waliona sio lazima.

Kwa mmoja wao, kuongeza neno hili itakuwa aibu. Kauli hizi ziliamsha hasira za psika wa Bunge ambaye alikataa kuahirisha mkutano huo licha ya kuongezeka taratibu kwa uchokozi wa majibizano hayo. Mapigano yalizuka kati ya wabunge kadhaa, yukio lililorushwa moja kwa moja hewani.

Nchini Jordan, wanawake walikuwa na haki ya kupiga kura mwaka 1974, miaka saba baada ya nchi nyingi jirani kama vile Syria, Misri na Yemen. 15% tu kati yao hufanya kazi. Hata hivyo ndio walio wengi kwenye vyuo vikuu lakini uzito wa utamaduni huo unabaki kuwa na nguvu sana. Mgogoro wa kiuchumi umewalazimu wanawake kushinda vikwazo vya kupata ajira. Hii inalazimisha jamii kubadilika bila shida.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.