Pata taarifa kuu

"Pandora Papers" yafichua majina ya viongozi kadhaa wanaokwepa kodi

Viongozi kadhaa, kiwa ni pamoja na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Czech, Mfalme wa Jordan au marais wa Kenya na Ecuador, wanamiliki kampuni au akaunti za benki za nje kukwepa kulipa kodi, kulingana na uchunguzi uliochapishwa Jumapili (Oktoba 3) na Jumuiya ya Kimataifa ya Wanahabari wa Upelelezi (ICIJ).

Mfalme Abdullah II wa Jordan na Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza Tony Blair wametajwa katika uchunguzi mpya kuhusu ukwepaji kodi uliofichuliwa Oktoba 3, 2021 na Jumuiya ya Kimataifa ya Wanahabari wa Upelelezi (ICIJ).
Mfalme Abdullah II wa Jordan na Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza Tony Blair wametajwa katika uchunguzi mpya kuhusu ukwepaji kodi uliofichuliwa Oktoba 3, 2021 na Jumuiya ya Kimataifa ya Wanahabari wa Upelelezi (ICIJ). AFP - YUSSEF ALLAN
Matangazo ya kibiashara

Uchunguzi huo unaoitwa "Pandora Papers" uliofanywa na Jumuiya ya Kimataifa ya Wanahabari wa Upelelezi (ICIJ) na timu ya vituo 150 vya habari, umegundua kuwa watu mashuhuri wapatao 330 ulimwenguni kote wanamiliki akaunti kama hizo za siri za nje ya nchi.

 

Baadhi ya viongozi wa sasa na wa zamani 35 na zaidi ya maafisa 300 wa umma wameonyeshwa kwenye faili kutoka kwa kampuni zilizosajiliwa katika mataifa ya nje , zilizopewa jina la Pandora Papers.

Familia ya Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, ambayo imetawala siasa za nchi hiyo tangu uhuru, ilimiliki kwa siri mtandao wa kampuni zilizofunguliwa katika maeneo yenye unafuu wa ulipaji ushuru kwa miongo kadhaa, kulingana na uvujaji mkubwa wa nyaraka za kifedha.

Kulingana na stakabadhi  hizi, Waziri Mkuu wa Czech Andrej Babis aliweka dola milioni 22 katika kampuni za nje ambazo zilitumika kufadhili ununuzi wa jumba kubwa la kifahari, Bigaud, huko Mougins, kusini mwa Ufaransa.

Stakabadhi hizo zilizovuja pia zinamhusisha Rais wa Urusi Vladimir Putin na mali za siri huko Monaco

Rais wa Ecuador Guillermo Lasso, mfanyakazi wa zamani wa benki, alibadilisha wakfu mmoja wa Panama ambao ulitoa malipo ya kila mwezi kwa wanafamilia wake wa karibu na amana iliyoko South Dakota nchini Marekani.

Nyaraka hizo zinaonyesha pia jinsi Mfalme wa Jordan alikusanya kwa siri mali ya thamani ya £ 70m Uingereza na Marekani

Baadhi ya waliotajwa wanakabaliwa na madai ya ufisadi, utakatishaji fedha na ukwepaji kodi ulimwenguni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.