Pata taarifa kuu
LEBANONI

Lebanon yatangaza serikali mpya, baada ya kusubiriwa kwa zaidi ya mwaka mmoja

Miezi 13 baada ya kujiuzulu kwa baraza la mawaziri la Hassan Diab, hatimaye Lebanon imepata serikali mpya Ijumaa hii (Septemba 10) itakayoongozwa na mwanasiasa kutoka dhehebu la Sunni na mfanyabiashara Najib Mikati. Serikali hiyo ina wajumbe 24, ambao wamegawanywa sawa kati ya Wakristo na Waislamu.

Waziri Mkuu wa Lebanon Najib Mikati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukutana na Rais wa Lebanon Michel Aoun katika Ikulu ya Rais huko Baabda, Lebanon, Septemba 10, 2021.
Waziri Mkuu wa Lebanon Najib Mikati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukutana na Rais wa Lebanon Michel Aoun katika Ikulu ya Rais huko Baabda, Lebanon, Septemba 10, 2021. REUTERS - MOHAMED AZAKIR
Matangazo ya kibiashara

Siku arobaini na tano baada ya kuteuliwa, Najib Mikati amefaulu pale ambapo Saad Hariri na, mtangulizi wake, Balozi Moustapha Adib walishindwa.

Mfanyabiashara huyo na Mbunge kutoka Tripoli, ambaye anachukua wadhifa wa Waziri Mkuu kwa mara ya tatu, aliweza kushinda moja kwa moja vizuizi vyote ambavyo vilikwamisha uundaji wa serikali na ambavyo vilishindwa kuzuia mchakato huo. Mazungumzo magumu yalikwama juu ya kugawana nyadhifa na uchaguzi wa mawaziri;

Rais Michel Aoun amekuwa akishtumiwa na wakosoaji wake kwamba alikuwa akitaka kupata theluthi moja ya nafasi za mawaziri. Lakini, katika baraza la mawaziri la Mikati hakuna chama kilicho na kizuizi hiki peke yake, kulingana na Waziri Mkuu.

Serikali mpya inapatikana kwa nchi hiyo iliyokumbwa na moja ya mzozo mbaya zaidi wa kiuchumi duniani tangu miaka 170, ambayo inakabiliwa na uhaba wa mafuta, dawa na vyakula kadhaa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.