Pata taarifa kuu
LEBANON-USALAMA

Lebanon: Watu kadhaa waangamia katika mlipuko wa lori la mafuta Akkar

Lori la kubeba mafuta limelipuka katika kijiji cha Tleil, katika mkoa wa Akkar, usiku wa Jumapili Agosti 15, 2021. Shirika la Msalaba Mwekundu nchini Lebanoni limesema watu wasiopungua 20 wamefariki dunia na wengine 80 wamejeruhiwa.

Eneo la mlipuko la lori ya mafuta huko Tleil, kaskazini mwa Lebanon. Mkoa wa Akkar, Jumapili Agosti 15, 2021.
Eneo la mlipuko la lori ya mafuta huko Tleil, kaskazini mwa Lebanon. Mkoa wa Akkar, Jumapili Agosti 15, 2021. AFP - GHASSAN SWEIDAN
Matangazo ya kibiashara

Shirika la Msalaba Mwekundu limebaini kwamba miili kadhaa imeteketea kwa moto, na ni vigumu kuwatambua raia waliofariki dunia. Makumi ya watu walio na majeraha mabaya walilazimika kupelekwa katika hospitali moja pekee ya mkoa inayotibu majeraha makubwa, katika jiji la Tripoli, kwenye umbali wa kilomita 25 kutoka eneo la tukio.

Mfanyakazi mmoja wa hospitali iliyo karibu na eneo tukio, Yassine Metlej, amelielezea shirika la habarila AFP kwamba "baadhi majeruhi nyuso zao zimeharibika sana, wengine hawana mikono tena". Hii ndio sababu hospitali hiyo ilikataa kuwapokea watu waliojeruhiwa kwa kukosa vifaa.

Picha zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha miili miili ya watu walioangamia katika mkasa huo, ikiwa ni pamoja na moto mmoja. Waziri Mkuu wa zamani Saad Hariri amebaini kwenye ukurasa wake rasmi wa Twitter kwamba "tukio la Akkar linafanana na lile lililotokea katika bandari Beirut", mwaka mmoja na siku kumi zilizopita huko. Ameomba serikali ya sasa kujiuzulu.

Ushahidi wa kwanza juu ya sababu za mlipuko

Kulingana na Chombo cha Habari cha kitaifa cha Lebanon (ANI), mkasa huo umetokana na lori la kubeba mizigo ambalo jeshi lilikuwa limekamata na ambalo lililipuka, baada ya makabiliano kati ya wakaazi waliokusanyika karibu ya gari ili kuweza kupata petroli. Jeshi halikuwepo katika eneo hilo wakati mlipuko huo ulipotokea, shirika hilo limesema.

Paul Khalifeh, mwandishi wetu huko Beirut, anaripoti kuwa mlipuko huo ulitokea bahati mbaya. Tukio hilo lilitokea baada ya kuondoka wanajeshi wa Lebanon waliokuwa wamekuja kukagua lori lililokuwa limesafirisha mafuta kinyume cha sheria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.