Pata taarifa kuu
LEBANON-SIASA

Rais Aoun atarajia serikali ndani ya masaa 48 wakati mgogoro ukizidi kutokota

Rais wa Lebanon Michel Aoun ameelezea matumaini yake kuwa serikali mpya itaundwa ndani ya masaa 48, kwani juhudi za kukubaliana juu ya muundo wa serikali ziliharakishwa na uhaba wa mafuta ambao umesababisha shughuli kuzorota kaika sehemu kubwa ya nchi, na kuchochea hofu ya kutokea kwa machafuko makubwa.

Rais wa Lebanon Michel Aoun wakati wa hotuba yake katika ikulu ya huko Baabda, Agosti 30, 2020.
Rais wa Lebanon Michel Aoun wakati wa hotuba yake katika ikulu ya huko Baabda, Agosti 30, 2020. Dalati Nohra/Handout via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Uhaba wa petroli umezidi kuwa mbaya na kuashiria mabadiliko mapya katika kuporomoka kwa uchumi wa Lebanon katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, kwani hospitali, viwanda vya mikate na biashara zingine zimelazimika kupunguza shughuli au kufunga wiki iliyopita.

Mwishoni mwa wiki, mlipuko wa gari la kubeba mafuta uliuwa watu wasiopungua 28 kaskazini mwa nchi, wakati wengi walikimbilia eneo la tukio kujaribu kupata mafuta.

Waziri Mkuu mteule Najib Mikati amesema baada ya mkutano na Michel Aoun kwamba bado kuna uwezekano kwamba serikali itaundwa ndani ya siku mbili zijazo.

Masuala tete yanajadiliwa moja baada ya nyingine, amesema, bila hata hivyo kuweza kuonyesha ni lini kikwazo cha mwisho kitaondolewa.

Kabla ya mazungumzo hayo, rais Aoun alikuwa amependekeza kwamba makubaliano yalikuwa karibu. "Tunakaribia kuunda serikali," alihakikishia Michel Aoun, kabla ya baadaye kutaja tarehe ya mwisho ya masaa 48.

Mazungumzo yanaenda katika mwelekeo sahihi, kulingana na chanzo cha juu cha kisiasa, ingawa maswali yanabaki kutatua - hasa utambulisho wa mawaziri.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.