Emmanuel Macron aahidi euro milioni 100 kusaidia raia wa Lebanon
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ameahidi kuwa serikali yake itatoa Euro Milioni 100 kama msaada wa dharura kwa nchi ya Lebanon, lakini pia dozi 500,000 za kukabiliana na janga la Covid-19.
Imechapishwa:
Rais Macron ametoa ahadi hiyo, katika kongamano la Kimataifa kuisaidia Lebanon kupata Dola Milioni 350 kulisaidia taifa hilo kuinuka kiuchumi.
Mwaka mmoja baada ya shambulio kwenye bandari ya Lebanon, nchi hiyo imekuwa katika kipindi kigumu cha kiuchumi, lakini pia imekuwa ikishuhudia changamoto za kisiasa.
Msaada huu utajikita hasa katika elimu, mahitaji ya chakula na kilimo, ametangaza rais wa Ufaransa, kwa kufungua mkutano huo kupitia njia ya video, akiwa mji wa Fort de Brégançon, huko Var (kusini-mashariki mwa Ufaransa). Mkutano ambao unafanyika kwa ushirikiano na Umoja wa Mataifa, mwaka mmoja baada ya mlipuko kwenye bandari ya Beirut.