Pata taarifa kuu
UTURUKI-MAREKANI-PALESTINA-ISRAEL-USHIRIKIANO

Viongozi wa nchi za Kiislamu wanakutana Istanbul kwa wito wa Erdogan

Viongozi wa nchi za Kiislamu wanakutana leo Jumatano Istanbul, nchini Uturuki kwa mkutano kuhusu uamuzi wa Marekani kutambua jerusalem kama mji mkuu wa Israel. Viongozi wao wanakutana kwa wito wa rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ambaye ana imani kuwa hatua kali zitachukuliwa.

Rais wa Uturuki katika mkutano wa Jumuyia ya nchi za Kiislam (OIC) tarehe 15 Aprili, 2016 Istanbul.
Rais wa Uturuki katika mkutano wa Jumuyia ya nchi za Kiislam (OIC) tarehe 15 Aprili, 2016 Istanbul. AFP
Matangazo ya kibiashara

Hatua ya rais Donald Trump ya kutambua mji mtakatifu wa Jerusalem kama mji mkuu wa nchi ya Kiyahudi wiki iliyopita imesababisha sintofahamu katika nchi za Kiarabu na kushtumiwa na nchi mbalimbali ulimwenguni, huku maandamano yakiibuka katika nchi kadhaa za Mashariki ya Kati.

Erdogan, mtetezi mkuu wa taifa la Wapalestina, alikuwa mmoja wa wakosoaji wa uamuzi huo wa Donald Trump, akilaani hatua ilio "kinyume na sheria ya kimataifa". Amesema Jerusalem, mji wa tatu mtakatifu wa Uislamu, " ni mstari mwekundu kwa Waislamu ambao haupaswi kuingiliwa ".

Erdogan ambaye ni rais wa Jumuiya ya nchi za Kiislamu (OIC), inayojumuisha nchi 57, ameitisha mkutano wa dharura ambapo ana imani kuwa atajaribu kuunganisha ulimwengu wa Kiislamu dhidi ya hatua hiyo ya rais Donald Trump.

Lakini kazi itakua ngumu,wakati ambapo ulimwengu wa Kiislamu umegawanyika na nchi kadhaa katika kanda ya Mashariki ya Kati, kama vile Saudi Arabia, zinajaribu kukuza mahusiano mazuri na utawala wa Trump dhidi ya kuongezeka kwa uhasama na nchi ya Iran.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.