Pata taarifa kuu
PALESTINA-ISRAEL-USALAMA

Wapalestina wawili wauawa Gaza, Israel yakanusha kuhusika kwake

Wapalestina wawili wameuawa katika Ukanda wa Gaza, huku mamlaka mjini Ramallah wakidai kuwa vifo hivyo vimesababishwa na shambulizi kutoka kwa wanajeshi wa Israel.

Sintofahamu yaibuka katika Ukanda wa Gaza na Ukingo wa Magharibi baada ya kutokea makabiliano kati ya waandamanaji na askari wa Israel.
Sintofahamu yaibuka katika Ukanda wa Gaza na Ukingo wa Magharibi baada ya kutokea makabiliano kati ya waandamanaji na askari wa Israel. REUTERS / Mohamad Torokman
Matangazo ya kibiashara

Jeshi la Israel hata hivyo limekanusha madai hayo, kwa kusema kuwa hawakuhusika kwa namna yeyote ile.

Wizara ya afya ya Palestina hata hivyo imesema watu wawili waliouawa ni wanaume waiwli waliolengwa wakiwa juu ya pikipiki.

Mauaji haya yamekuja wakati huu, hali ya wasiwasi ukiendelea kuwepo kuanzia wiki iliyopita, baada ya Marekani kutangaza kutambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel.

Hatua hii imewakasirisha Wapalestina ambao wamesema imepoteza matumaini ya upatikanaji wa amani kati yake na Palestina.

Kwa siku ya tano leo kumekuwa na maandamano katika mamlaka ya Palestina na mataifa mengine ya Kiislamu na Kiarabu kulaani hatua huyo.

Israel kwa upande wake, imeendelea kusisitiza kuwa amani ya kweli na Palestina inaweza kupatikana iwapo mji wa Jerusalem utatambuliwa na kila mmoja kuwa makao makuu ya nchi yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.