Pata taarifa kuu
RWANDA-SIASA-HAKI

Kesi ya Diane Rwigara kuanza kusikilizwa Kigali

Kesi dhidi ya Mwanasiasa wa upinzani Diane Rwigara, inaanza leo jijini Kigali. Rwigara mwenye umri wa miaka 37, anakabiliwa na mashtaka ya uhaini na udanganyifu.

Diane Rwigara (watatu kutoka kushoto) na mama yake wakati kesi yao ikiahirishwa, Septemba 24, 2018 Kigali, Rwanda.
Diane Rwigara (watatu kutoka kushoto) na mama yake wakati kesi yao ikiahirishwa, Septemba 24, 2018 Kigali, Rwanda. Cyril NDEGEYA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Kuelekea kuanza kwa kesi hii, mwanasiasa huyo ameliambia Shirika la Habari la Ufaransa AFP kuwa, Rwanda ni kama jela.

Mpema mwezi Oktoba Mahakama ya Rwanda iliamuru kuachiliwa kwa Diane Rwigara, anayeonekana kama mwiba kwa utawala wa Rais Paul Kagame, baada ya kuzuiliwa yeye na mama yake kwa muda wa zaidi ya mwaka mmoja kwa kusubiri kesi yake.

Diane Rwigara anakabiliwa na madai ya kughushi stakabadhi katika kujaribu kuwania uchaguzi wa urais mnamo mwezi Agosti 2017 na kuchochoea uasi. Wakati huo alikamatwa yeye na mama yake.

Kosa la kuchochea uasi linaadhibiwa kwa kifungo cha miaka 15. na kosa la kughushi stakabadhi linaadhibiwa kwa kifungo cha miaka 7 nchini Rwanda.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.