Pata taarifa kuu

Kenya: Wanasayansi wana wasiwasi kuhusu kiwango cha kutisha cha kuongezeka kwa maji

Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi wa Baharini ya Kenya ilitoa tahadhari mwishoni mwa juma. Msimu mrefu wa mvua umeanza na nchi, kama eneo zima, kwa mara nyingine tena inakabiliwa na mvua kubwa, kutokana na mfumo wa hali ya hewa unaojulikana kama El NiΓ±o.

(Pcha ya kielelezo) Waendesha pikipiki huvuka barabara iliyojaa maji baada ya mvua kubwa kunyesha Mombasa, Kenya, Novemba 3, 2023.
(Pcha ya kielelezo) Waendesha pikipiki huvuka barabara iliyojaa maji baada ya mvua kubwa kunyesha Mombasa, Kenya, Novemba 3, 2023. AFP - SIMON MAINA
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu mjini Nairobi, GaΓ«lle Laleix

Mitaa iliyogeuzwa kuwa mito, magari yanayoelea kama boti, mikahawa ikiwa imemezwa na maji... Pwani ya Kenya kwa mara nyingine tena inakabiliwa na mafuriko.

Hali hii ya kupanda kwa viwango vya maji ilianza wiki jana, inaeleza Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi wa Bahari ya Kenya. Iliimarishwa siku ya Alhamisi kwa mwezi mpya na upepo mkali ambao ulisababisha mawimbi ya zaidi ya mita 4 kwenda juu.

Lakini tatizo halisi ni El Nino: mfumo wa hali ya hewa ya mzunguko ambayo husababisha mvua kubwa kutoka Bahari ya Pasifiki. Mvua katika siku za hivi karibuni nchini Kenya ilijaza mito ya nyanda za juu, ambayo sasa inabeba maji mengi, viwango ambavyo Bahari ya Hindi inashindwa kupokea.

Kwa mujimbi wa Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi, Kenya haikuwa imekumbana na ongezeko kama hilo la viwango vya maji tangu 1997/1998, miaka ambayo pia ilikumbwa na mfumo wa hali ya hewa unaojulikana kama El NiΓ±o.

Kiuhalisia, nchi zote za Kiafrika katika Bahari ya Hindi ziko hatarini kukumbwa na mmomonyoko wa ardhi. Kulingana na taasisi ya hali ya hewa ya IGAD, shirika la kikanda la Pembe ya Afrika, Bahari ya Hindi huongezeka kwa karibu 5 mm kwa mwaka, wakati wastani wa kimataifa ni 3 mm.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.