Pata taarifa kuu
RWANDA-SIASA-HAKI-USALAMA

Diane Rwigara na mama yake waachiliwa huru kwa dhamana Rwanda

Mahakama ya Rwanda imeamuru kuachiliwa kwa mwanasiasa wa upinzani nchini humo Diane Rwigara, anayeonekana kama mwiba kwa utawala wa Rais Paul Kagame, baada ya kuzuiliwa yeye na mama yake kwa muda wa zaidi ya mwaka mmoja kwa kusubiri kesi yake.

Mwanasiasa wa upinzani nchini Rwanda Diane Rwigara.
Mwanasiasa wa upinzani nchini Rwanda Diane Rwigara. REUTERS/Jean Bizimana
Matangazo ya kibiashara

Diane Rwigara, 37, anakabiliwa na madai ya kughushi stakabadhi katika kujaribu kuwania uchaguzi wa urais mnamo mwezi Agosti 2017 na kuchochoea uasi. Wakati huo alikamatwa yeye na mama yake.

Majaji watatu wamebaini kwamba upande wa mashtaka yalishindwa kutoa ushahidi wa kuaminika ili kuendelea kuwazuia watuhumiwa hao wawili na hivyo kuamuru kuachiliwa huru kwa dhamana.

Uamuzi huu umepokewa kwa vifijo na nderemo kutoka kwa jama na familia waliokuwepo mahakamani. Hata hivyo Diane Rwigara na mama yake wamepigwa marufuku kusafiri kwenda nje ya mji wa Kigali na wametakiwa kukabidhi pasipoti zao kwa mamlaka husika.

Kesi yao inatarajia kuanza tena mwezi Novemba. Kosa la kuchochea uasi linaadhibiwa kwa kifungo cha miaka 15. na kosa la kughushi stakabadhi linaadhibiwa kwa kifungo cha miaka 7.

Dada ya Diana, Anne Rwigara, ambaye alizuiliwa kwa muda mfupi na watuhumiwa hao mwaka jana na baadaye kuachiliwa kwa kukoesekana uchahidi, amekaribisha hatua hiyo. "Hawana hatia na tunajua kwamba mashtaka dhidi ya dada yangu na mama yangu ni ya uongo na kwamba mashitaka hayo yalitengenezwa kwa sababu za kisiasa".

Uamuzi huu pia umekaribishwa na viongozi wa upinzani nchini Rwanda, kama vile Victoire Ingabire, ambaye hivi karibuni alipata msamaha wa rais baada ya kutumikia miaka minne jela baada kuhukumiwa kufungwa jela miaka kumi na tano kwa kosa la uhaini na kupinga mauaji ya kimbari.

"Kukamatwa kwa Rwigara yalikuwa ni mambo ya kisiasa na ninafurahi kuwa yeye na mama yake walmeachiliwa huru (...) Ni ishara kwamba Rwanda inaanza kupiga hatua nzuri katika masuala ya kisiasa ", Victoire Ingabire ameliambia shirika la Habari la AFP.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.