Pata taarifa kuu

Kenya : Mkuu wa majeshi aliyefariki katika ajali ya helikopta amezikwa Jumapili

Nchini Kenya, Mkuu wa Majeshi ya ulinzi, Francis Omondi Ogolla aliyefariki pamoja na maafisa wengine tisa wa jeshi baada ya kuanguka kwa helikopta ya kijeshi wiki hii, amezikwa jana nyumbani kwake kwenye kijiji cha Mor, katika Kaunti ya Siaya, Magharibi mwa nchi hiyo.

Wanajeshi wa Jeshi la Ulinzi la Kenya (KDF) wakiwa karibu na jeneza la mkuu wa jeshi la Kenya, Jenerali Francis Ogolla, aliyefariki katika ajali ya helikopta ya kijeshi wakati wa ibaada katika uwanja wa Ulinzi Sports Complex huko Langata jijini Nairobi, Kenya Aprili 20, 2024. REUTERS/Thomas Mukoya
Wanajeshi wa Jeshi la Ulinzi la Kenya (KDF) wakiwa karibu na jeneza la mkuu wa jeshi la Kenya, Jenerali Francis Ogolla, aliyefariki katika ajali ya helikopta ya kijeshi wakati wa ibaada katika uwanja wa Ulinzi Sports Complex huko Langata jijini Nairobi, Kenya Aprili 20, 2024. REUTERS/Thomas Mukoya REUTERS - Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Malefu ya waombolezaji wakiongozwa na rais William Ruto, walihudhuria mazishi hayo.

Maafisa wakuu wa jeshi, walimpa heshima za mwisho, kwa kupigwa miziga 19 kwa ajili ya kiongozi wao.

Soma piaJenerali Francis Ogola alikuwa nani?

Rais William Ruto amemkumbuka kama kiongozi mahiri na shupavu wa Majeshi ya ulinzi ya Kenya, na kusisitiza kuwa hakuwahi kujutia kumteua kwenye nafasi hiyo.

‘‘Nilijivunia sana kufanya kazi na Jenerali Ogolla ambapo kwenye mikono yake usalama wa Kenya ulikuwa dhabiti.’’ alieleza rais William Ruto.

00:29

Rais William Ruto kuhusu Jenerali Francis Ogolla

Aidha, Ruto amewaahidi Wakenya kuwa ukweli utabainika kuhusu kilichosababisha kuanguka kwa helikopta ya kijeshi iliyosababisha kifo cha Jenerali Ogola.

‘‘Nina imani kubwa na generali Omenda na tume yake kuwa watafanya uchunguzi wa kina kubaini hasa nini kilisababisha ajali iliopelekea kifo cha Jenerali Ogola.’’ alisisitiza rais Ruto.

00:15

Rais William Ruto kuhusu Jenerali Francis Ogolla ajali

Jenerali Ogola, aliyeteuliwa kwenye nafasi hiyo mwezi Aprili mwaka uliopita, amepoteza maisha kwenye ajali hiyo ya helikopta akiwa na umri wa miaka 62 akiwa kwenye ziara ya kikazi, katika êneo la Elgeyo Marakwet, linalosumbuliwa na utovu wa usalama kutokana na kuwepo wa wezi wa mifugo.

Florence Kiwuwa- Rfi Kiswahili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.