Pata taarifa kuu

DRC: Marekani inaamini mzozo wa DRC unapaswa kutatuliwa kwa njia ya mazungumzo

Marekani kupitia maafisa wake wawili walioitembelea DRC mwishoni mwa juma lililopita inasema inaamini kuwa mgogoro wa kivita unaoshuhudiwa mashariki mwa nchi hiyo unapaswa kutatuliwa kwa njia ya mazungumzo.

Raia wa mashariki ya DRC wamekuwa wakikabiliwa na changamoto za kiusalama kutoka kwa makundi ya waasi.
Raia wa mashariki ya DRC wamekuwa wakikabiliwa na changamoto za kiusalama kutoka kwa makundi ya waasi. REUTERS - ARLETTE BASHIZI
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa wajumbe hao wawili wa Marekani ambao ni Enrique Roig, naibu katibu msaidizi wa serikali katika ofisi kuu inayojihusisha na demokrasia, utawala na amani katika Idara inayosimamia majimbo, na Mark Billera, naibu msimamizi katika ofisi kuu na yenyewe ikiwa yenye kusimamia demokrasia ya USAID, ni kuwa matumizi ya silaha huko mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo inayoshuhudiwa haiwezi kusuluhisha mgogoro kati ya serikali ya Kinshasa na waasi wa M23.

Waasi wa M23 wamekuwa wakituhumiwa kutekeleza mashambulio dhidi ya raia mashariki wa DRC.
Waasi wa M23 wamekuwa wakituhumiwa kutekeleza mashambulio dhidi ya raia mashariki wa DRC. AP - Moses Sawasawa

Maafisa Hao wawili wa Marekani walithibitisha hayo siku ya Jumamosi ya Aprili 20 mjini Kinshasa, mwishoni mwa ziara ya wiki moja ambapo walitembelea mamia kwa maelfu ya wakimbizi kwenye makambi nchini DRC.

Enrique Roig aliwaambia waandishi wa habari mjini Kinshasa kwamba wanafanya kazi na maafisa Wa Congo lakini pia na washirika wa kikanda kutafuta suluhu ya matatizo ya Mashariki mwa nchi hiyo, na kwamba anafahamu jukumu lililotekelezwa na M23, chini ya vikwazo vya kimataifa kundi ambalo amekiri linaungwa mkono na Rwanda, huku akithibitisha kuwa wamihimiza nchi ya Rwanda kukubali kuwaondoa mara moja wanajeshi wake nchini DRC na kumwajibisha mtu yeyote anayetuhumiwa kufanya ukiukaji wa haki za binadamu.

Ruben Lukumbuka- Rfi Kiswahili

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.