Pata taarifa kuu

Mvua yasababisha mafuriko makubwa jijini Nairobi, uharibifu waripotiwa

Nchini Kenya, jiji kuu la Nairobi linashuhudia mafuriko makubwa kutokana na mvua inayoendelea kunyesha, kama ilivyo kwenye nchi jirani za Afrika Mashariki.

Mafuriko nchini Kenya
Mafuriko nchini Kenya © REUTERS - STRINGER
Matangazo ya kibiashara

Barabara zimejaa maji, huku baadhi ya mitaa iliyo Mashariki mwa jiji hilo, ikifurika na kusababisha wakaazi kushindwa kuingia wala kuondoka.

Serikali inasema tangu mvua kubwa ilipoanza kunyesha mwezi Aprili, watu zaidia ya 30 wamepoteza maisha nchini humo, likiwemo jiji kuu Nairobi.

Mamlaka ya utabiri wa hali ya hewa nchini humo, imekuwa ikitoa tahadhari ya kushuhudia kwa mvua kubwa, na sasa inasema mbali na mafuriko, huenda kukashuhudiwa maporomoko ya ardhi.

“Mvua itaendelea kunyesha sana. Tuna mashaka kuwa huenda kukatokea na maporomoko ya ardhi,” amesema, David Gikungu,  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo.

Serikali inasema imechukua tahadhari kuwasaidia raia wa nchi hiyo, waliothiriwa.

“Maafisa wetu wa uokoaji wapo katika maeneo yaliyoathiriwa kuwasaida, watu walioathirika,” amesema naibu msemaji wa serikali Gabriel Mutuma.

01:28

GABRIEL MUTHUMA MINI MODULE 24 04 2024

Pius Masai mtalaam wa kukabiliana na majanga nchini Kenya, anasema serikali ndio ya kulaumiwa baada ya mafuriko kujaa mitaani.

“Maafisa wa serikali walikuwa wapi, wakati wananchi walipokuwa wanajenga kwenye mkondo wa maji ?,” amehoji katika mazungumzo yake na RFI Kiswahili.

02:46

MODULE PIUS MASAI KUHUSU MAFURIKO

Mvua kubwa zinazoendelea kunyesha pia zimetatiza shughuli za kawaida katika miji mingine ya Afrika Mashariki kama Dar es salaam nchini Tanzania, ambako barabara zimejaa maji, sawa na Bujumbura huku tahadhiri ikitolewa kwa wakaazi kuchukua tahadhri na kuhamia maeneo yaliyoinuka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.