Pata taarifa kuu

Mafuriko yazidi kuwatatiza raia nchini Kenya,mvua kubwa ikiendelea kunyesha

Mafuriko yameendelea kuripotiwa katika maeneo tofauti nchini Kenya kutokana na mvua kubwa inayoendelea kunyesha, makaazi ya watu yakifurika, usafiri pia ukiripotiwa kutatizika jijini Nairobi na miji mingine ambapo pia vifo vimeripotiwa.

Mwanamume akiongoza mifugo wake kwenye maji ya mafuriko huko Kisumu, Kenya Jumatano, Aprili 17, 2024. Mvua kubwa inayonyesha katika maeneo tofauti ya Kenya imesababisha vifo vya takriban watu 13 na wengine 15,000 kuwa wakimbizi, Umoja wa Mataifa ulisema, huku watabiri wa hali ya hewa wakionya mvua kubwa itaendelea hadi Juni. (Picha ya AP/Brian Ongoro)
Mwanamume akiongoza mifugo wake kwenye maji ya mafuriko huko Kisumu, Kenya Jumatano, Aprili 17, 2024. Mvua kubwa inayonyesha katika maeneo tofauti ya Kenya imesababisha vifo vya takriban watu 13 na wengine 15,000 kuwa wakimbizi, Umoja wa Mataifa ulisema, huku watabiri wa hali ya hewa wakionya mvua kubwa itaendelea hadi Juni. (Picha ya AP/Brian Ongoro) AP - Brian Ongoro
Matangazo ya kibiashara

Mwandishi wetu wa Mombasa Diana wanyonyi anasimulia hasara ilitokana mafuriko hayo pwani ya Kenya.

Bonea Kone, ni mkulima kutoka kijiji cha Kone Masa, anayekadiria hasara ya zaidi ya shilling laki tano za Kenya baada shamba lake la ekari 16 kuharibiwa na mafuriko kutoka Mto Tana.

‘‘Hii watermelon huenda ikakosa boti iozee hapo hapo, tunataka usaidizi kutoka kwa serikali kwa hali na mali. ’’alisemaBonea Kone, ni mkulima kutoka kijiji cha Kone Masa.

00:05

Bonea Kone, ni mkulima kutoka kijiji cha Kone Masa

Barisa Dido ni mkulima mwingine anasimulia hali ilivyo.

‘‘Nimeathirika na maji, shamba ekari sita ya watermelon, ekari moja ya butternuts na ekari moja ya pojo, haya maji yametuletea shida hatuna njia. ’’alieleza Barisa Dido ni mkulima.

00:09

Barisa Dido ni mkulima mwingine

Baadhi ya wafanyibiasha hapa wametoka eneo la Nairobi na huko Meru katika eneo la mlima Kenya, walifika eneo hili kununua vyakula kutoka kwa wakulima, lakini kwa sasa wanakadiria hasara.

Sisi tulifika hapa tangu Jumatatu, mizogo yenye tulikuwa tumekata ikakwama kule mashambani kule ng’ambo. Boti ni chache gari ni mingi, sisi wanunuzi tuko wengi. Kule ndani kuna gari zaidi ya kumi- zimesimama huko na hakuna matumaini ya kutoka kwa sababu maji yamefika na imekuwa mto.’’ Walisema baadhi ya baadhi ya wafanyibiasha.

00:17

Wafanyibiashara walioathirika na mafuriko

Wakaazi hapa wanahofia kuwa huenda wakapata maambukizo yanayosababishwa na mafuriko hayo.

‘‘Haya maji yako na harufu mbaya na shida ya haya maji yanatuletea madhara ya tumbo haswa.’’ Mmoja wa wakaazi alieleza.

 

00:17

Raia wanaohofia magonjwa kutokana na mafuriko

 

Wakaazi kutoka vijiji 11 huenda wakalazimika kuhama makaazi yao kufuatia ongezeko la maji itokanayo kwa mvua.

Diana Wanyonyi, Mombasa – RFI, KISWAHILI.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.