Pata taarifa kuu
RWANDA-MAJANGA-USALAMA

Watu zaidi ya 40 wapoteza maisha kufuatia mvua kubwa Rwanda

Mvua kubwa ambazo zimekuwa zikinyesha nchini Rwanda zimesababisha vifo vya zaidi ya watu 40 na kuharibu mashamba. Serikali ya Rwanda imesisitiza wananchi wake kuhama maeneo ya mabondeni.

Mvua zilizonyesha kwa siku 30 mfululizi, zimesababisha maafa makubwa ikiwa ni pamoja na vifo vya watu, mifugo, huku mashamba na nyumba vikiharibiwa vibaya.
Mvua zilizonyesha kwa siku 30 mfululizi, zimesababisha maafa makubwa ikiwa ni pamoja na vifo vya watu, mifugo, huku mashamba na nyumba vikiharibiwa vibaya. RFI/Stéphanie Aglietti
Matangazo ya kibiashara

Katika kipindi cha mwezi mmoja peke , watu 41 wamepotza maisha nchini Rwanda kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha kwa wingi. Mvua zilizonyesha kwa siku 30 mfululizi, zimesababisha maafa makubwa ikiwa ni pamoja na vifo vya watu, mifugo, huku mashamba na nyumba vikiharibiwa vibaya.

Walioathiriwa zaidi na majanga haya ni wakazi wa kaskazini mwa Rwanda na kusini, kwani takwimu kutoka wizara ya Majanga zinaonesha kuwa nusu ya walioathirika wametoka maeneo hayo.

Wakazi wa maeneo hayo wanasema kwamba msimo ujao huenda mavuno yakawa si mazuri na wanakabiliwa na janga la njaa.

Mafuriko haya hayatofautiani na yale yaliyotokea mwaka 2016 ambapo wakati huo serikali ilisema kuwa, itafanya kila liwezekanalo mafuriko kama hayo hayaathiri tena wananchi.

Serikali ya Rwanda imeandaa namna ya kuwasaidia watu waliokumbwa na majanga, mtu yeyote atakayeakumbwa na majanga atasaidiwa, lakini tunatoa wito kwa wale wanaoishi katika maeneo hatari, kuyahama makazi yao haraka iwezekanavyo, amesema Habinshuti Philippe afisa kwenye wizara ya majanga MIDIMAR.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.