Pata taarifa kuu
Tanzania

Kenya, Rwanda na Uganda zatoa msaada kwa wahanga wa tetemeko Tanzania

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo Jumamosi Septemba 17, amepokea taarifa ya maafa yaliyosabaishwa na tetemeko la ardhi lililotokea hivi karibuni na kuathiri vibaya mji wa Bukoba mkoani Kagera, sambamba na michango ya fedha na vifaa mbalimbali kutoka kwa marais wa Uganda, Kenya na Rwanda

Athari za tetemeko la ardhi mjini Bukoba Tanzania
Athari za tetemeko la ardhi mjini Bukoba Tanzania RFI/Martha Saranga
Matangazo ya kibiashara

Rais Magufuli amepokea fedha taslimu kiasi cha dola laki mbili sawa na Shilingi za Kitanzania takribani Milioni Mia nne na thelathini na saba (Tshs-437,000,000/-) kutoka kwa Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Museveni sambama na taarifa ya mchango wa mabati, blanketi na magodoro vyenye thamani ya Shilingi za Kitanzania milioni 115 kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta.

Akizungumza baada ya kupokea taarifa ya maafa na michango kwa ajili ya waathirika wa maafa hayo, Rais Magufuli amewashukuru rais Museveni, Kenyata na Kagame ambao wamempigia simu za kumpa pole na tayari wametoa misaada yao, pamoja na wote waliojitoa kusaidia waathirika wa tetemeko hilo.

Aidha rais Magufuli ametoa wito kwa Watanzania na watu mbalimbali walioguswa na maafa haya kuendelea kutoa misaada kwa waathirika kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera, huku akionya na kuvitaka vyombo vya dola kuwafuatilia watu wanaotaka kutumia maafa haya kukusanya michango kwa lengo la kujinufaisha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.