Pata taarifa kuu
BURUNDI - RWANDA

Burundi yaishushia lawama mpya Serikali ya Rwanda

Chama tawala nchini Burundi cha CNDD-FDD, kimeishambulia tena kwa maneno nchi jirani ya Rwanda kwa kupinga ukweli wa kuwepo kwa mauaji ya kimbari ya mwaka 1994, kikisema kuwa ni mbinu ya walioko madarakani kujipa uhalali dhidi ya serikali ya Kihutu iliyokuwepo jijini Kigali chini ya Rais Juvenal Habyarimana.

Mmoja wa msanii akiwa na kishada cha upepo chenye rangi za chama Tawala, CNDD-FDD, cha Rais Pierre Nkurunziza
Mmoja wa msanii akiwa na kishada cha upepo chenye rangi za chama Tawala, CNDD-FDD, cha Rais Pierre Nkurunziza AFP PHOTO / CARL DE SOUZA
Matangazo ya kibiashara

Kauli hiyo imetolewa na mwenyekiti wa chama hicho katika taarifa ya wiki iliyopita, ambapo sanjari na hayo aliishutumu nchi ya Canada kusaidia mipango ya uvamizi wa Burundi, wakati ambapo waziri wa ulinzi wa nchi hiyo akitamatisha ziara yake katika ukanda wa maziwa makuu.

Hii ni mara nyingine kauli nzito inatolewa na upande wa Burundi kuelekea Rwanda, baada ya tuhuma kwamba Rwanda inawahifadhi na kuwasaidia waasi wa Burundi waliojaribu kupindua serikali ya Rais Pierre nkurunziza tarehe 13 mwezi Mei mwaka 2015 mjini Bujumbura chini ya uongozi wa aliyekuwa mkuu wa usalama wa taifa Jenerali Godefroi Niyombare.

Akizungumzia hali ilivyo baina ya nchi hizo mbili alipohojiwa na mwandishi mmoja wa habari mjini Rubavu alipompokea mwenzake wa DRC Rais joseph kabila Kabange, Rais Paul Kagame wa Rwanda alisema kuwa anatumaini kuwa busara ya Kabila kama mwenyekiti wa Jumuiya ya Uchumi ya nchi za maziwa makuu CEPGL itasaidia kuboresha uhusiano huo.

Tangu wiki kadhaa, Burundi imepiga marufuku mabasi yaliyokuwa yanaenda Rwanda kuvuka mpaka wake na kuzuia chakula kisivuke mpaka.

Kwa vyovyote hivyo, hatma ya uhusiano baina ya Burundi na Rwanda sasa iko kitanzini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.