Pata taarifa kuu
BURUNDI-USALAMA

Msuluhishi wa kitaifa Burundi arejea nchini

Baada ya zaidi ya miezi kumi akiwa nje ya nchi kwa sababu za matibabu, Msuluhishi wa kitaifa nchini Burundi, Mohammed Khalfan Rukara, hatimaye amerejea nchini, huku kukiwa na uvumi kuwa aliitoroka nchi akihofia usalama wake.

Mohammed Rukara, Msuluhishi wa kitaifa Burundi.
Mohammed Rukara, Msuluhishi wa kitaifa Burundi. www.assemblee.bi
Matangazo ya kibiashara

Rukara anarejea nchini wakati hali ya usalama bado ni tete na mazungumzo kati ya wadau wote chini ya upatanishi wa rais wa zamani wa Tanzania, Benjamin Mkapa, yakioonekana kutopewa uzito wowote, kwa mujibu wa wadadisi.

Hayo yanajiri wakati, raia kutoka maeneo mbalimbali ya nchi hio, hasa wakazi wa mji wa Bujumbura wamekua wakilalamika kuhusu kupanda mara dufu kwa bei za bidhaa mahitajio, huku kukionekana kuzuka kwa magenge ya watu wenye silaha ambao wameanza kuwaibia raia mali na vitu vyao wakiwakuta majumbani kwao ifikapo jioni.

Hayo yanajiri wakati ambapo serikali ya Burundi imepiga marufuku chakula kutoka Burundi kuingia nchini Rwanda. Uamuzi huo ulitangazwa Jumamosi hii na Makamu wa pili wa rais Joseph Butore alipokua akiwahutubia raia baada ya shughuli ya kujitolea ya kusafisha miji wilayani Rugombo mkoani Cibitoke, kilomita 10 na mpaka wa Rwanda.

Uhusiano kati ya nchi hizi mbili umeendelea kudorora kwa mwaka mmoja sasa, ambapo serikali ya Bujumbura inaishtumu serikali ya Kigali kuyafadhili makundi ya waasi kwa lengo la kuuwangusha utawala wa Pierre Nkurunziza, jambo ambalo serikali ya Kigali inakanusha.

Rwanda inawapa hifadhi wakimbizi wa Burundi karibu laki moja, huku wengine wakitawanyika katika nchi za Tanzania, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Kenya, Uganda, Zambia na Malawi. Zaidi ya wakimbizi wa Burundi 280,000 wamelazimika kukimbilia nje ya nchi wakihofia usalama wao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.