Pata taarifa kuu
BURUNDI

Human Rights Watch yasema kundi la Imbonerakure limewabaka wanawake Burundi

Shirika la Kimataifa la kutetea haki za Binadamu la Human Rights Watch, linasema kundi la vijana la Imbonerakure la chama tawala nchini Burundi CNDD-FDD limekuwa likiwabaka  wanawake na wasichana tangu mwaka uliopita.

Raia Burundi wakiyakimbia makwao kutokana na mzozo wa kisiasa nchini humo
Raia Burundi wakiyakimbia makwao kutokana na mzozo wa kisiasa nchini humo AFP Photo/Oxfam/Mary Mndeme
Matangazo ya kibiashara

Ripoti ya shirika hilo inasema, wanawake na wasichana waliobakwa na kundi hili ni wale walionekana kuipinga serikali ya rais Piere Nkurunziza.

Aidha, ripoti hiyo imeeleza kuwa mbali na vijana hao maafisa wa polisi walihusika na ubakaji huo na walionekana wakiwa wamevalia sare zao.

Ripoti nyingine kama hii ilitolewa na Tume ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa mwezi Januari mwaka huu.

Wanawake 13 waliohojiwa katika nyakati tofauti wamekiri kubakwa na makundi hayo yanayoiunga mkono serikali, madai ambayo serikali jijini Bujumbura imekuwa ikikanusha.

Burundi ilianza kushuhudia mgogoro wa kisiasa mwaka uliopita, baada ya rais Piere Nkurunziza kuamua kuwania urais kwa muhula wa tatu.

Machafuko nchini humo yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 500 na zaidi ya 200,000 wakikimbilia mataifa jirani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.