Pata taarifa kuu

Kenya: Charles Muriu Kahariri ateuliwa kuwa Mkuu wa jeshi (KDF)

Rais wa Kenya William Ruto siku ya Alhamisi amemteua Charles Muriu Kahariri kuwa mkuu wa jeshi baada ya kifo cha mtangulizi wake, Francis Omondi Ogolla, katika ajali ya helikopta mwezi uliopita.

Charles Muriu Kahariri, aliyepandishwa cheo hadi cheo cha jenerali, alikuwa anashikilia wadhifa wa naibu wa Francis Omondi Ogolla (kwenye picha).
Charles Muriu Kahariri, aliyepandishwa cheo hadi cheo cha jenerali, alikuwa anashikilia wadhifa wa naibu wa Francis Omondi Ogolla (kwenye picha). AFP - LUIS TATO
Matangazo ya kibiashara

Jenerali Ogolla na maafisa wengine tisa wa kijeshi waliuawa Aprili 18 katika ajali ya helikopta katika eneo la mbali kaskazini-magharibi mwa Kenya. Nchi hii ilianza siku tatu za maombolezo siku iliyofuata.

Charles Muriu Kahariri, aliyepandishwa cheo hadi cheo cha jenerali, alikuwa anashikilia wadhifa wa naibu wa Francis Omondi Ogolla.

Aliyekuwa naibu kamanda wa Jeshi la Wanamaji la Kenya, Bw. Kahariri alijiunga na kikosi cha ulinzi cha Kenya mnamo mwezi Aprili 1987, na akapanda daraja wakati wa "kazi yake adhimu iliyochukua zaidi ya miongo mitatu", kulingana na taarifa iliyotolewa na Wizara ya Ulinzi.

Mwanamume huyu ana mke na baba wa watoto watatu alishiriki kama kamanda wa kitengo cha baharini katika uvamizi wa Wakenya nchini Somalia mwaka wa 2011 uliolenga kuwaondoa wanamgambo wa Kiislamu wa Al Shabab.

Operesheni hii ya kijeshi ilifuatia utekaji nyara wa raia wanne wa kigeni, wakiwemo wafanyakazi wawili wa mashirika ya kutoa misaada wa Uhispania, kutoka kambi kubwa ya wakimbizi karibu na mpaka.

Mhitimu wa Chuo cha Vita vya Majini nchini Marekani, alikuwa kamanda wa kikosi kazi cha operesheni iliyochukua udhibiti wa ngome ya Al Shabab huko Kismayo, bandari ya kimkakati ambayo ilikuwa "kitovu cha kibiashara" cha wanamgambo wa Kiislamu wa Somalia.

Rais wa Kenya pia alimteua Fatuma Gaiti Ahmed kama mkuu wa jeshi la anga, mwanamke wa kwanza katika historia ya Kenya kushikilia wadhifa huu. Anachukua nafasi ya John Mugaravai Omenda, aliyepandishwa cheo na kuwa naibu mkuu wa majeshi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.