Pata taarifa kuu
BURUNDI-JESHI-USALAMA

Uchunguzi wabaini Askari wa Burundi walitoroka jeshi ugenini

Baadhi ya asklri wa Burundi waliotumwa kutekeleza majukumu yao katika nchi za kigeni wamekua wakiamua kutorudi nchini mwao baada ya kukamiliza majukumu yao kufuatia hali inayoendelea nchini Burundi.

Askari wakipiga doria mjini Bujumbura, Mei 2, 2015.
Askari wakipiga doria mjini Bujumbura, Mei 2, 2015. REUTERS/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Wengi wao ni maafisa ambao bado ni vijana, wakibaini kwamba wanahofia kuuawa baada ya kujikuta kuwa majina yao yamewkwa kwenye orodha ya watu ambao wanatafutwa na utawala wa Pierre Nkurunziza.

Askari hao wanasema kuwa wameamua kuchukua uamuzi wa kutorudi nchini Burundi kufuatia opereshenni ya kimya kimya ya kuwakamata baadhi ya askari wanaomaliza majukumu yao katika nchi za kigeni ambako walikotumwa, wakishtumiwa kuwa karibu na upinzani. Operesheni hiyo imekua ikiwalenga maafisa wa jeshi na polisi ambao bado ni vijana kutoka jamii ya Watutsi, kwa mujibu wa ripoti kadhaa za mashirika yasiyo ya kiserikali na Umoja wa Mataifa. Kwa mujibu wa taarifa zilizokusanywa na RFI, maafisa 14 ikiwa ni pamoja na maafisa wa ngazi ya juu katika jeshi na polisi tayari wametangaza kutorudi nyumbani na kuomba hifadhi katika nchi za kigeni.

* Thomas ni afisa wa jeshi ambaye bado, akiwa katika majukumu yake ya kikazi katika nchi ya Pembe la Afrika. Ameamua kukaidi amri ya viongozi wake na kutorudi nyumbani kwa sababu ya ukandamizaji unaoendelea kushiuhudiwa nchini Burundi: "Operesheni ya kamakama kiholela, mateso, mauaji ya watu walio mikononi mwa vyombo vya dola vinatekelezwa na maafisa wa Idara ya Ujasusi na wanamgambo wa chama madarakani cha CNDD-FDD (Imbonerakure), [vijana wa chama tawala]. Vijana hao wamechukua nafasi ya utawala kwa kuwakamata wanajeshi wa Burundi, hasa wale kutoka jamii ya Watutsi na maafisa vijana. Wanafanya mashambulizi dhidi ya familia zao kuwazuia, kuwatusi, kuwatesa na wakati mwingine kuwaua. "

Kwa mujibu wa ripoti kadhaa za mashirika yasiyo ya kiserikali, maafisa wa Kitutsi wanalengwa hasa na ukandamizaji huo. Tarehe 12 Agosti 2016, Kamati ya Umoja wa Mataifa dhidi ya mateso ilisema kutiwa "wasiwasi na ripoti thabiti zinazoeleza mauaji na kupotezwa kwa maafisa wa zamani wa vikosi vya jeshi la Burundi," askari wa jeshi la zamani lililokua likiongozwa na Watutsi. Taarifa zinazoendana sambamba na ripoti kadhaa za Tume ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa katika miezi ya karibuni.

Thomas na wenzake watatu wanadai kuona majina yao katika orodha ya wanajeshi wanaotakiwa kufuatilia kwa karibu. Wanasema orodha hiyo waliiona ikisambazwa katika mitandao ya kijamii na tayari wamefanyiwa vitishona askari wenzao. Kwa hiyo wamechukua uamuzi wa kulitoroka jeshi na kutorudi nyumbani: "Tuna hofu ya kukamatwa kama ilivyokuwa kwa askari aliyekamatwa katika uwanja wa ndege wa Bujumbura wakati alipokua akirudi baada ya kukamilisha majukumu yake ya kikazi nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, siku chache zilizopita" Thomas amesema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.