Pata taarifa kuu

Watalii waokoloewa Kenya, idadi ya vifo yafikia watu 181 kutokana na mafuriko

Takriban watalii zaidi ya mia moja waliokuwa wamekwama kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa katika hifadhi maarufu ya Maasai Mara kusini magharibi mwa Kenya wameondolewa, msimamizi wa eneo hilo amesema.

Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya limesema limewaokoa watu 61 waliokuwa wamekwama kwenye kambi, zaidi ya nusu yao kwa njia ya anga.
Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya limesema limewaokoa watu 61 waliokuwa wamekwama kwenye kambi, zaidi ya nusu yao kwa njia ya anga. AP - Edaward Odero
Matangazo ya kibiashara

Mvua kubwa iliyosababishwa na mfumo wa hali ya hewa uitwao El Niño, tayari imesababisha mafuriko makubwa katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki, na kusababisha uharibifu wa barabara, madaraja na miundombinu mingine. Takriban watu 179 wamefariki katika majanga yanayohusiana na mafuriko tangu mwezi Machi, kulingana na takwimu rasmi.

"Kuna watalii zaidi ya mia moja" waliokwama katika zaidi ya nyumba kumi na mbili za kulala wageni na kambi, Stephen Nakola, msimamizi wa kitongoji cha Narok Magharibi, aliliambia mapema Jumatano shirika la habari la AFP. "Hii ni takwimu ya awali kwa sababu kambi nyingi hazifikiki," amesema.

Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya limesema limewaokoa watu 61 waliokuwa wamekwama kwenye kambi, zaidi ya nusu yao kwa njia ya anga. "Katika kambi zingine, mahema yalichukuliwa" wakati daraja lilihariiwa, amesema kwenye mtandao wa X.

Hifadhi ya Maasai Mara ina utajiri mkubwa wa wanyamapori wakiwemo simba, tembo, faru, chui, twiga, viboko na duma, ambao huvutia watalii kutoka pande zote za dunia.

Wakati wa usiku kuanzia Jumapili hadi Jumatatu, bwawa la asili katikati mwa Kenya lilipasuka kutokana na athari za mvua zinazoendelea kunyesha, na kutoa kijito chenye nguvu cha maji ya matope ambacho kilisomba vijiji kadhaa; karibu watu 50 walifariki, tukio baya zaidi tangu kuanza kwa msimu wa mvua.

Kama majirani zake wengi wa Afrika Mashariki, Kenya inakumbwa na msimu wa mvua wenye vurugu kutokana na mfumo wa hali ya hewa uiitwao El Niño ambayo huongeza mvua.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.