Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-HAKI

Rwanda: Mpinzani Victoire Ingabire hajaidhinishwa kugombea urais (mahakamani)

Mahakama ya Rwanda leo Jumatano Machi 13 imefutilia mbali ombi la kurejesha haki za kiraia za Victoire Ingabire, mwanasiasa wa upinzani nchini Rwanda na mkosoaji wa Rais Paul Kagame, uamuzi ambao unamzuia kugombea katika uchaguzi wa urais wa Julai 15.

Victoire Ingabire, mwanasiasa wa upinzani nchini Rwanda na mkosoaji wa Rais Paul Kagame.
Victoire Ingabire, mwanasiasa wa upinzani nchini Rwanda na mkosoaji wa Rais Paul Kagame. AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Mwanasiasa huyo wa upinzani mwenye umri wa miaka 55, ambaye hawezi kukata rufaa dhidi ya uamuzi huu kabla ya miaka miwili, alinyang'anywa haki yake baada ya kupatikana na hatia na kuhukumiwa mwaka 2013 kifungo hadi miaka 15 jela kwa "kula njama dhidi ya mamlaka kupitia ugaidi na vita" na "kupuuzia mbali mauaji ya kimbari ya 1994" , ambayo yalisababisha vifo vya watu 800,000 kati ya mwezi Aprili na Julai 1994, hasa miongoni mwa Watutsi walio wachache.

Mwishoni mwa Juma lililopita rais anayemaliza muda wake nchini Rwanda, Paul Kagame, aliidhinishwa na chama chake ca RPF kuwania muhula mwingine Julai 15, siku moja kabla ya mwaasiasa wa upinzani Frank Habineza kutangaza kuingia kwenye kinyang'anyiro hicho, akifahamu kukosekana kwa usawa wa pande husika. Licha ya vitisho, kufungwa na kukimbilia uhamishoni, Habineza alisema anakataa kunyamazishwa.

Frank Habibeza, 47, alikihama chama tawala cha Rwandan Patriotic Front (RPF) mwaka 2009 na kuunda chama chake, Green Democratic Party. Kujitolea kwake kisiasa kulimletea vitisho, kufungwa jela na kukimbilia uhamishoni.

Uchaguzi wa Julai utampa tena ushindi Paul Kagame, aliye madarakani tangu mwaka 2000.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.