Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-DEMOKRASIA

Rais wa Rwanda Paul Kagame kuwania urais kwa mara ya 4

Chama tawala cha Rwanda, Rwandan Patriotic Front (RPF), siku ya Jumamosi kimemteua Rais wa nchi hiyo Paul Kagame kuwa mgombea wake wa uchaguzi wa urais wa Julai 15, kwa muhula wa nne wa miaka saba.

Paul Kagame, Rais wa Rwanda, katika mkutano na waandishi wa habari kzbla ya kufunga mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Madola mjini Kigali, Juni 25, 2022.
Paul Kagame, Rais wa Rwanda, katika mkutano na waandishi wa habari kzbla ya kufunga mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Madola mjini Kigali, Juni 25, 2022. REUTERS - JEAN BIZIMANA
Matangazo ya kibiashara

FPR imebaini kwamba imemchagua, bila upinzani, wakati wa kongamano lililomalizika Jumamosi. Paul Kamage, 66, ameitawala Rwanda kwa mkono wa chuma tangu katikati ya miaka ya 1990 na kushinda uchaguzi wa urais, kila mara kwa zaidi ya 90% ya kura, katika chaguzi za mwaka 2003, 2010 na 2017.

Mmoja wa washindani wake wachache katika uchaguzi wa urais ni kiongozi wa chama cha upinzani cha Green Party, Frank Habineza.

Mbunge mwenye umri wa miaka 47, alipata asilimia 0.45 pekee ya kura katika uchaguzi wa urais wa mwaka 2017. Anawekwa nafasi ya tatu kwa chunguzi za sasa, zikikosolewa na vyama vya kutetea haki za binadamu kwa makosa yao na vitisho katika uchaguzi dhidi ya wapiga kura.

Mshindani mwingine anayewezekana wa Bw. Kagame, Victoire Ingabire, kiongozi wa vuguvugu ambalo halijasajiliwa la Dalfa Umurunzi (Maendeleo na Uhuru kwa Wote), katika hatua hii ameondolewa kwenye kinyang'anyiro cha urais kutokana na kuhukumiwa hapo awali.

Uamuzi wa mahakama uliopangwa kufanyika Machi 13 ndio utakaoamua iwapo ameidhinishwa kuwania urais au la.

Rwanda inapanga uchaguzi wake wa urais na wa wabunge Julai 15, kulingana na uamuzi wa mwaka jana wa serikali wa kufanya uchaguzi katika tarehe hiyo.

Wabunge 24 wanawake, wawakilishi wawili wa vijana na mwakilishi mmoja wa Wanyarwanda wenye ulemavu pia watachaguliwa na vyuo na kamati za uchaguzi mnamo Julai 16.

Wagombea wataweza kufanya kampeni kuanzia Juni 22 hadi Julai 12, kulingana na tume ya uchaguzi.

Rwanda inajionyesha kama moja ya nchi zilizo na utulivu katika bara la Afrika, lakini mashirika kadhaa ya haki za binadamu yanamshutumu Bw. Kagame kwa kuitawala katika mazingira ya hofu, kukandamiza upinzani na uhuru wa kujieleza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.