Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-SIASA

Mpinzani wa Rwanda Frank Habineza yuko tayari kwa uchaguzi wa urais 'usio na usawa'

Wakati rais anayemaliza muda wake nchini Rwanda, Paul Kagame, akiwania muhula mwingine Julai 15, mwaasiasa wa upinzani Frank Habineza anaingia kwenye kinyang'anyiro hicho, akifahamu kukosekana kwa usawa wa pande husika. Licha ya vitisho, kufungwa na kukimbilia uhamishoni, Habineza anakataa kunyamazishwa.

Mgombea urais, mwanasiasa wa upinzani Frank Habineza wa chama cha upinzani cha Green Democratic Party, wakati wa mkutano wa kampeni za uchaguzi wilayani Musanze, Rwanda, Julai 28, 2017.
Mgombea urais, mwanasiasa wa upinzani Frank Habineza wa chama cha upinzani cha Green Democratic Party, wakati wa mkutano wa kampeni za uchaguzi wilayani Musanze, Rwanda, Julai 28, 2017. © AP
Matangazo ya kibiashara

Mkuu wa chama pekee kilichoidhinishwa kinachokosoa mamlaka nchini Rwanda, kiongozi mkuu wa upinzani, Frank Habineza anagombea kwa mara ya pili katika uchaguzi wa urais mwezi Julai. Frank Habineza anawania tena uchaguzi wa urais Julai 2024, licha ya " muktadha wa uchaguzi usio na usawa" unaompendelea rais anayemaliza muda wake Paul Kagame.

Mgombea pekee aliyetangazwa kwa sasa na rais anayeondoka, Frank Habineza anajua kwamba mazingira ya uchaguzi hayatakuwa "ya haki". Kinyang'anyiro hicho "hakina usawa kwetu", anabaini, akikashifu hasa ubabe wa FPR, chama tawala, kinachosimamia kila kitu ikiwemo tume ya uchaguzi. "Huwezi kubadilisha chochote kwa kukaa nje ya uwanja, ukishangilia mechi," anasema mtu ambaye alipata 0.45% ya kura mnamo mwaka 2017: "Lazima uwe ndani ya mfumo, kupamana na mfumo."

Frank Habibeza, 47, alikihama chama tawala cha Rwandan Patriotic Front (RPF) mwaka 2009 na kuunda chama chake, Green Democratic Party. Kujitolea kwake kisiasa kulimletea vitisho, kufungwa jela na kukimbilia uhamishoni.

Uchaguzi wa Julai utampa tena ushindi Paul Kagame, aliye madarakani tangu mwaka 2000. Habineza anafahamu vikwazo vya kugombea kwake, hasa ubabe wa RPF dhidi ya tume ya uchaguzi. Licha ya mazingira mabaya, Habineza anakataa kukaa kimya. Ushiriki wake unalenga kuvunja ukimya na kuhimiza kuibuka kwa upinzani wa kweli nchini Rwanda.

Dhamana ya upinzani

Mpango wa Habineza unasisitiza kuheshimiwa kwa haki za binadamu, uhuru wa kujieleza na kupunguza umaskini. Pia anashutumu makubaliano yenye utata na London kuhusu kutumwa kwa wahamiaji nchini Rwanda.

Chama cha Green Democratic Party kilipokea idhini kutoka kwa mamlaka kabla ya uchaguzi wa wabunge wa mwaka 2013, na kilipata viti viwili vya Bunge mwaka wa 2018. Ingawa kinakosoa mamlaka, wakati mwingine kinadaiwa kuwa ni uidhinishaji wa upinzani, usio na madhara kwa utawala wa Kigali.

"Tulipigania kile tulicho nacho," anatetea Frank Habineza, akisisitiza kwamba baadhi ya wanachama wa chama "bado wanaishi uhamishoni." "Tulipinga mabadiliko ya katiba" yaliyopitishwa mwaka 2015 kuruhusu Paul Kagame kusalia madarakani hadi mwaka 2034, anaongeza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.