Pata taarifa kuu

Mafuriko nchini Kenya: Vitongoji duni vyabomolewa ili kulazimisha watu kuhama

Nchini Kenya, kimbunga Hidaya kilipoteza nguvu nyingi kilipofika pwani ya Tanzania Jumamosi Mei 4. Upepo umekaribia kupungua lakini mamlaka ya hali ya hewa nchini Kenya bado linaonya kuhusu mvua kubwa siku hizi.

Wakazi wa Nairobi wakijaribu kukusanya mali zao kufuatia mafuriko nchini Kenya, Aprili 25, 2024. (Picha ya kielelezo)
Wakazi wa Nairobi wakijaribu kukusanya mali zao kufuatia mafuriko nchini Kenya, Aprili 25, 2024. (Picha ya kielelezo) © Monicah Mwangi / REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu mjini Nairobi, Albane Thirouard

Mvua kubwa kwa bahati mbaya imekuwa mara kwa mara kwa Wakenya katika miezi ya hivi majuzi. Idadi ya vifo na majeruhi kutokana na mafuriko inaendelea kuongezeka. Watu 219 wamekufa na zaidi ya 200,000 kuhama makazi yao. Kukabiliana na hali hii, serikali imeagizwa raia kuhamishwa kutoka maeneo yote yaliyo hatarini. Maeneo kadhaa ya mji mkuu yameathirika.

Makaazi yasiyo rasmi kwenye maeneo ya pembezoni mwa mto tayari yamebomolewa ili kulazimisha watu kuhama. Maelfu ya watu walijikuta mitaani, kulingana na mashirika ya ndani.

Makaazi kadhaa yalibomolewa siku ya Jumamosi Mei 4, kando ya mto katika mtaa wa mabanda wa Mukuru kwa Reuben, jijini Nairobi. 

Tingatinga zilikuwa zikisonga mbele na kuharibu kila kitu. Nyumba yangu ambayo ilikuwa hapa na biashara yangu iliharibiwa. Walitupa dakika 15 tu kuhama,” amesema David Mwangi Maina.

Wakazi kadhaa wanasema walilala usiku katika makazi ya muda. Gladys Muraa alilala kwenye magofu ya nyumba yake, pamoja na mama yake na watoto sita: “Hatujahama tangu jana kwa sababu hatujui pa kwenda. Tulilala njaa. Mvua zinaendelea lakini hatuna chakula, hatujapata msaada, hakuna. "

Hakuna makazi mapya

Wakazi wamesema kuwa bado hawajapokea ofa ya kujengewa nyumba jana alasiri.

Anami Daudi Toure, mratibu wa Kituo cha Haki ya Kijamii cha kitongoji hicho, anapinga: “Hatua pekee ambayo serikali imechukua kukabiliana na hatari ya mafuriko katika kitongoji hicho ni kuwahamisha wakazi. Hawakutoa misaada ya kibinadamu, hakuna chakula, maji au dawa. Kile ambacho mamlaka ilipaswa kufanya ni kuandaa orodha ya wakazi na kuweka pamoja mpango wa kuwahamisha kwa ubinadamu. "

Akikabiliwa na shutuma nyingi kutoka kwa upinzani, Mjumbe wa Waziri wa Mambo ya Ndani alitembelea eneo hilo siku ya Jumamosi. Aliwahakikishia kuwa familia hizo zitahamishwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.