Pata taarifa kuu
VIKWAZO-USALAMA

EU yatangaza vikwazo dhidi ya wanasiasa na viongozi wa makundi yenye silaha DRC

Umoja wa ulaya umetangaza kuwawekea vikwazo viongozi wa makundi yenye silaha pamoja na mwanasiasa Justin Bitakwira ambaye pia aliwahi kuhudumu kama waziri wa zamani wa maendeleo nchini DRC.  

Maafisa wa usalama wakiwa Ituri, Mashariki mwa DRC
Maafisa wa usalama wakiwa Ituri, Mashariki mwa DRC SAMIR TOUNSI / AFP
Matangazo ya kibiashara

Baraza la Umoja wa Ulaya, EU, limesema limeamua kuwaongeza watu wanane katika orodha ya watu waliowekewa vikwazo, akiwemo mfanyabiashara maarufu wa dhahabu  raia wa Ubelgiji Alain Goetz. 

Wengine ni pamoja na msemaji wa waasi wa M23, Willy Ngoma, na viongozi wengine wa makundi ya waasi ya ADF, CODECO, FDLR, Mai Mai na afisa mmoja wa jeshi la DRC. 

Mwanasiasa Justin Bitakwira ambaye pia aliwahi kuwa Waziri, yupo pia kwenye orodha hiyo kwa tuhma za kuchochea chuki dhidi ya kabila la Banyamulenge huko Minembwe.  

Enock Ruberangabo Sebineza mmoja wa wakilishi wa Kabila hilo la Banyamulenge na mbunge wa zamani kutoka eneo hilo anasema wameikaribisha hatua hiyo ya Umoja wa Ulaya.  

Wengi wao wanatuhumiwa kwa kuhusika na ukiukwaji mkubwa wa haki za biandamu pamoja na kuendeleza vita nchini RDC, huku wengine wakiorodheshwa kwa misingi ya kuchochea ghasia na kuanzisha vita, na kujihusisha na biashara haramu.  

Jumla ya watu 17 sasa wako chini ya vikwazo vya EU, ambapo wamepigwa marufuku ya kuingia barani Ulaya, na mali zao kuzuiliwa. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.