Pata taarifa kuu

Ripoti ya Umoja wa Mataifa MONUSCO: Zaidi ya raia 130 wauawa na waasi wa DRC

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, uchunguzi wa awali uliofanywa na Tume ya Umoja wa Mataifa nchini humo MONUSCO, umebaini kuwa waasi wa M 23 waliwauwa raia 131 kati ya tarehe 29 na 30 katika kijiji cha Kishishe, mwezi uliopita, katika jimbo la Kivu Kaskazini.

Hali nayojiri Mashariki mwa Jamhuri a Kidemokrasia ya Kongo.
Hali nayojiri Mashariki mwa Jamhuri a Kidemokrasia ya Kongo. © REUTERS - James Akena 2
Matangazo ya kibiashara

Aidha, ripoti ya MONUSCO imeeleza kuwa waasi hao waliwabaka pia wanawake na wasichana, madai ambayo  waasi hao wamekanusha. 

Umoja wa Mataifa unasema wahasiriwa walinyongwa katika kile kinachoonekana kuwa kulipiza kisasi mashambulizi ya sasa ya serikali.

Ripoti hii inakuja wakati huu, serikali ya DRC ikisema, waasi hao waliwauwa raia 300 katika shambulio hilo, wakiwemo watoto. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.