Pata taarifa kuu

Viongozi wa Pakistan, Iran na Afghanistan wakubaliana kupambana na ugaidi

Rais wa Afghanistan Hamid Karzai ameuambia mkutano wa kimataifa wa kupambana na ugaidi kuwa mbali na juhudi za serikali yake,bado ugaidi umeendelea kushika kasi nchini Afghaniatan na kuwa tishio nchini mwake na kwa mataifa mengine.

Raisi wa Afghanistan Hamid Karzaï
Raisi wa Afghanistan Hamid Karzaï Reuters
Matangazo ya kibiashara

Karzai amewaambia viongozi ndani ya kutano huo kuwa Amani ya nchini Afghanistan ni tete kwa hivyo nchi zote zisaidie juhudi za kupambana na ugaidi.

Akigusia hatua ya rais wa Marekani Barack Obama kuondoa vikosi vyake nchini Afghanistan ,Karzai amesema serikali yake iko tayari kurithi mikoba hiyo na kuahidi kuimarisha ulinzi nchini mwake,huku akisifu kuwa hatua ya Obama ni faida kwa taifa la marekani na Afghanistan.

Siku ya jumatano Obama alitangaza kuwa kikosi cha askari elfu kumi wataondoka nchini Afghanistan mwaka huu na wengine elfu thelathini na tatu wataondoka ifikapo mwakani kipindi cha majira ya joto.

Mkutano huo wa siku mbili umehudhuriwa na viongozi wa nchi takriban sita zikiwemo Afghanistan,Iran na Pakistan.

Wakati hayo yakijiri,watu takriban 30 wameuawa kwa bomu la kujitoa muhanga na wengine 45 wamejeruhiwa katika hospitali moja kusini mwa mji wa Kabul nchini Afghanistan maafisa nchini humo wamethibitisha.

Kundi la wanamgambo wa Taliban wamekana kuhusika na shambulio hilo huku msemaji wake Zabihullah Mujahid akikemea kitendo hicho na kuongeza kuwa shambulio hilo limefanyika ili kulichafua kundi hilo.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.