Pata taarifa kuu
MAANDAMANO-UCHUMI

'Wacha tuishi!' : Wanigeria wamechoshwa na mfumuko wa bei na umaskini

Maelfu ya waandamanaji wamekusanyika kwa amani siku ya Jumanne asubuhi katika miji mitatu mikuu ya Nigeria kupinga gharama kubwa ya maisha, ambayo imelipuka tangu rais mpya aingie madarakani chini ya mwaka mmoja uliopita.

Waandamanaji wakikusanyika karibu na makao makuu ya Bunge la taifa la Nigeria wakati wa maandamano huko Abuja mnamo Februari 27, 2024.
Waandamanaji wakikusanyika karibu na makao makuu ya Bunge la taifa la Nigeria wakati wa maandamano huko Abuja mnamo Februari 27, 2024. © Kola Sulaimon / AFP
Matangazo ya kibiashara

Huko Lagos (kusini), mji mkuu wa kiuchumi, Abuja (katikati), mji mkuu wa shirikisho, na Kano (kaskazini), jiji la pili kwa watu wengi zaidi nchini, Wanigeria elfu kadhaa waliingia mitaani kwa wito wa shirikisho la vyama vya wafanyakazi, Nigeria Labour Congress (NLC), kushutumu mageuzi ya Rais Bola Ahmed Tinubu, ambayo yamesababisha mlipuko wa gharama ya maisha.

Huko Abuja, maelfu ya waandamanaji walikusanyika mbele ya Bunge la taifa, wakipeperusha bendera na ishara za muungano wakidai "kukomeshwa kwa kushuka kwa thamani ya naira" na "waache maskini wapumue".

"Tunakusanyika kwa sababu ya umaskini na ukosefu wa usalama," alisema Patrick Madu, 44 na baba wa watoto watano, ambaye analazimika kufanya kazi kama dereva wa teksi pamoja na kazi yake ya ujenzi. "Hatuna chakula cha kutosha nyumbani," anasema Mercy Adeyemi, mwenye umri wa miaka 48 na mwanachama wa NLC, ambaye anasema akula kwa mlo mmoja ili kujikimu.

Alipoingia madarakani Mei 2023, Rais Bola Tinubu alikomesha ruzuku ya mafuta na udhibiti wa sarafu, na kusababisha kupanda mara tatu kwa bei ya petroli na kupanda kwa gharama ya maisha, naira kupoteza thamani yake kwa kasi dhidi ya dola. Kiwango cha mfumuko wa bei nchini humo kilikaribia asilimia 30 mwezi Januari na maandamano kadhaa tayari yamefanyika tangu mwanzoni mwa mwezi wa Februari katika miji midogo midogo kaskazini na katikati mwa nchi.

Rais wa Nigeria amerudia kuwataka wakazi kuwa na subira, akibaini kwamba mageuzi yake ya kiuchumi yatawavutia wawekezaji wa kigeni na kufufua uchumi, lakini matokeo chanya ya mageuzi haya ni yanachelewa kuonekana. Hata kama idadi ya waandamanaji katika miji mitatu mikuu itasalia kuwa ya dhihaka katika nchi hii yenye wakazi zaidi ya milioni 220, maaandamano hayo yananaonyesha hali halisi kwa ujumla na idadi ya watu wa Nigeria ambao wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula.

“Kuwa ombaomba”

Wanigeria wengi wamelazimika kuacha vyakula vinavyochukuliwa kuwa vya anasa, kama vile nyama, mayai, maziwa na viazi. Angalau 63% ya Wanigeria wanaishi katika umaskini uliokithiri, kulingana na takwimu rasmi. "Hali ya kiuchumi inazidi kutovumilika, gharama ya maisha ni kubwa zaidi kuliko tunachopata, tumekuwa ombaomba," anabaini Habibu Idris katikati ya waandamanaji 500 waliokusanyika katika jimbo la Kano.

Huko Lagos, chini ya waandamanaji 2,000 waliosindikizwa na kikosi kikubwa cha polisi waliandamana kwa amani hadi kwenye ofisi za gavana wa jimbo hilo, wakiimba "Mwizi wa Tinubu!".

"Tinubu aliahidi mabadiliko na sasa angalia tulipo? Hakuna chakula, hakuna usalama katika nchi hii," anasema Aghedo Kehinde Stephen, mwanachama wa mashirika ya kiraia. “Inatosha, hakuna tumaini tena kwetu hapa,” anabaini Abiodun Olamide Thomas, muuguzi mwenye umri wa miaka 35 ambaye anasema “yuko tayari kuhamia ng’ambo fursa ikitokea.”

Chini ya shinikizo kutoka kwa watu wengi kutoridhika, serikali ilitangaza siku ya Jumatatu kuanza kwa mpango wa msaada unaolenga kutoa naira 25,000 kwa mwezi (takriban euro 14.70) kwa milioni 15 za kaya maskini zaidi nchini humo. Hii haikuzuia NLC kuitisha maandamano mengine siku ya Jumatano.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.