Pata taarifa kuu

Mgogoro wa chakula wasababisha Wanigeria kuingia mitaani

Maisha ya kila siku ya Wanigeria wengi yamezorota kwa kasi kutokana na kupanda kwa bei ya vyakula, na kuwalazimu kuruka milo na kula mchele usio na ubora, ambao hapo awali ulikuwa wa kulisha samaki.

Watu hununua chakula katika soko huko Owo, kusini-magharibi mwa Nigeria, Juni 7, 2022.
Watu hununua chakula katika soko huko Owo, kusini-magharibi mwa Nigeria, Juni 7, 2022. © AP
Matangazo ya kibiashara

 

Kwa wiki kadhaa, wakaazi wa miji kadhaa katikati na kaskazini mwa nchi wamejitokeza barabarani kuelezea hasira zao. Wiki iliyopita, huko Suleja, karibu na mji mkuu Abuja, katikati mwa nchi, mamia ya waandamanaji waliandamana mitaani wakiwa wamebeba mabango yaliyosomeka: "Wanaigeria wanateseka."

Huko Minna, katika jimbo la Niger (kaskazini-kati), waandamanaji walifunga barabara na huko Kano (kaskazini), jiji la pili kwa idadi kubwa ya watu nchini Nigeria, na wanawake walishutumu bei ya juu ya unga.

Video zilizorushwa kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha wanawake wa Nigeria kaskazini mwa nchi wakichimba ardhini kwa ajili ya mbegu zilizohifadhiwa na mchwa ili kulisha watoto wao.

Tangu aingie madarakani mwaka jana, Rais wa Nigeria Bola Ahmed Tinubu amemaliza ruzuku ya mafuta na udhibiti wa sarafu, na kusababisha kupanda mara tatu kwa bei ya petroli na kupanda kwa gharama ya maisha, pesa ya naira kupoteza thamani yake kwa kasi dhidi ya dola.

Kiwango cha mfumuko wa bei nchini Nigeria kilifikia rasmi 28.92% mwezi Desemba, kiwango chake cha juu zaidi katika miaka mitatu.

Raia wa Nigeria wanapambana na "matatizo ya kiuchumi, njaa na njaa iliyokithiri", amir wa kitamaduni mwenye ushawishi mkubwa wa Kano, Aminu Ado Bayero, alisema siku ya Jumatatu, akimtaka rais kuchukua hatua za dharura.

Angalau 63% ya watu milioni 220 wa Nigeria wanaishi katika umaskini uliokithiri, kulingana na takwimu rasmi.

Wanigeria wengi wamelazimika kuacha vyakula vinavyochukuliwa kuwa "bidhaa za anasa", kama vile nyama, mayai, maziwa na viazi.

Mchele kwa ajili ya kuishi

Huko Kano, wakazi wamegeukia mchele wa bei nafuu, wa ubora wa chini unaoitwa "afafata," ikimaanisha "kupigana" katika lugha ya Kihausa na inarejelea matumizi yake katika nyakati ngumu.

Gharama ya unga wa mahindi, mtama na ulezi pia imeongezeka, na 80% ya nafaka inazalishwa kaskazini magharibi na kaskazini mashariki mwa nchi, lakini ukosefu wa usalama katika mikoa hii umeongeza shinikizo kwa wakulima.

Uvamizi mbaya na utekaji nyara kwa ajili ya fidia unaofanywa na magenge ya wahalifu kaskazini-magharibi mwa nchi na mizozo ya wanajihadi kaskazini-mashariki kumesababisha jamii nyingi za wakulima kuyahama makazi yao.

Nigeria pia ilifunga mpaka wake wa kaskazini na Niger baada ya mapinduzi ya kijeshi yaliyomwondoa madarakani rais Mohamed Bazoum mwaka jana, na kuzuia mtama na kunde kufika sokoni kaskazini mwa Nigeria.

"Tulinde vijiji vyetu"

Waziri wa Kilimo wa Nigeria Abubakar Kyari aliliambia Bunge siku ya Jumatatu kwamba usalama wa chakula nchini humo uko chini ya mkazo kufuatia janga la UVIKO-19 na mafuriko makubwa.

Lakini kulingana na Ya'u Tumfafi, meneja katika soko la nafaka la Dawanau, katika viunga vya Kano, tatizo liko kwingineko: "watu matajiri wameanza kuuza nafaka ambazo wanazihifadhi kwa wingi katika maghala".

Ili kukabiliana na hali ya kutoridhika inayoongezeka, Rais Tinubu aliagiza kutolewa kwa tani 102,000 za nafaka kutoka kwa hifadhi ya kimkakati ili kuuzwa kwa kiwango cha ruzuku ili kupunguza bei ya chakula.

Huko Kano, mamlaka ilivamia maghala ambapo wafanyabiashara wanashukiwa kuhifadhi chakula. Mapema mwezi huu, serikali ya Jimbo la Yobe ilipiga marufuku ununuzi wa wingi wa nafaka katika masoko ya ndani.

Gavana wa Jimbo la Niger Mohammed Umar Bago siku ya Ijumaa alitangaza kupiga marufuku ununuzi wa vyakula kwa wingi katika masoko ya ndani, na kuamuru vikosi vya usalama kunyang'anya malori yaliyokuwa yamebeba bidhaa nyingi na "kugawana chakula na wakazi.

Lakini kwa mfanyabiashara wa nafaka Ya'u Tumfafi, hizi ni "hatua za kutuliza." "Je, tani 102,000 zinaweza kusaidi nini kwa watu milioni 220?"

"Acha serikali ihifadhi vijiji vyetu kaskazini-magharibi na kaskazini mashariki ili watu waweze kurejea na kulima mashamba yao," amesema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.