Pata taarifa kuu
KATIBA-USALAMA

DRC: Mjadala juu ya uwezekano wa mabadiliko ya Katiba uko mezani

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Katiba inatarajiwa kujadiliwa hsawa kuhusu uwezekano wa mabadiliko. Kwa mujibu wa maelezo ya mwisho, Félix Tshisekedi alichaguliwa tena kwa muhula wa pili na wa mwisho mnamo mwezi wa Desemba 2023. Lakini katika siku za hivi karibuni, wakati wa mikutano na diaspora barani Ulaya, rais wa Kongo hajasema wazi kuhusu mjadala wa marekebisho ya Katiba.

Picha ya kielelezo] Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Félix Tshisekedi, wakati wa mkutano na waandishi wa habari katika ikulu ya Élysée, mjini Paris, Aprili 30, 2024.
Picha ya kielelezo] Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Félix Tshisekedi, wakati wa mkutano na waandishi wa habari katika ikulu ya Élysée, mjini Paris, Aprili 30, 2024. AFP - CHRISTOPHE ENA
Matangazo ya kibiashara

Hizi ni kauli mbili za rais wa Kongo wiki hii wakati wa ziara yake barani Ulaya ambazo zimeibua mjadala. Huko Paris, kwanza, Jumatano Mei 1 jioni, mbele ya diaspora, Félix Thisekedi alihojiwa na umma juu ya swali hili. "Msinifanye dikteta," alijibu, kabla ya kuongeza: "Mtazamo huu sio suala langu tu, bali la raia kupitia wawakilishi wao katika Bunge la taifa."

Siku mbili baadaye, Ijumaa Mei 3, huko Brussels, mbele ya diaspora, rais alienda mbele kidogo. "Nitaunda tume ambayo itatafakari kwa utulivu jinsi ya kutupatia Katiba inayostahili nchi yetu," alibainisha.

Mstari mwekundu kwa upinzani

Mabadiliko haya ya Katiba ni mstari mwekundu ambao tayari umeonya upinzani nchini DRC. Kambi ya Moïse Katumbi pia imetangaza kwamba jukumu lake katika Bunge litakuwa sehemu ya kuzuia jaribio lolote la kurekebisha Katiba hii.

Na kwa upande wa mashirika ya kiraia, kiongozi wa Asadho, Jean-Claude Katende, anabaini kwa upande wake, katika ujumbe kwenye mitandao ya kijamii, kwamba "Katiba hii inabakia kuwa chombo pekee kinachowaleta Wakongo pamoja" na kwamba "kipaumbele" badala yake ni "kulinda Mashariki ya nchi".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.