Pata taarifa kuu

Morocco: Maimamu kumi na watatu waliotumwa Ulaya kwa ajili ya Ramadhani watoweka

Maimamu ambao waliondoka nchini Moroco ili kueneza “neno jema” kwa Wamorocco wanaoishi Ulaya katika mfumgo wa mwezi mtukufu wa Ramahani, hawakurudi kamwe nchini humo. Maimamu kumi na watatu, waliotumwa Ufaransa, Ubelgiji na Ujerumani na Wizara ya Masuala ya Kidini ya Morocco kwa mwezi wa Ramadhani "walitoweka" walipokuwa wakijianda kurejea nchini.

Sala ya Lailatu Al-qadr (Usiku wa cheo) huko Rabat, Morocco (picha ya kielelezo).
Sala ya Lailatu Al-qadr (Usiku wa cheo) huko Rabat, Morocco (picha ya kielelezo). AFP - FADEL SENNA
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu huko Rabat, Victor Mauriat

Maimamu hao wana shahada ya kwanza, shahada ya uzamili au hata udaktari. Wanalipwa kila mwezi na serikali ya Morocco kwa kufanya kazi katika msikiti wao na kunufaika na safari ya kwenda na kurudi, hadi Ulaya kuongoza sala ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, gharama zote zinalipwa na serikali ya Morocco.

Hata hivyo, mwishoni mwa mwezi huu mtukufu kwa Waislamu, tarehe 12 Aprili, maimamu wasiopungua kumi na watatu waliotumwa na Wizara ya Habbous na Masuala ya Kiislamu hawakufika kwenye uwanja wa ndege na tangu wakati huo wametoweka.

Mchakato wa uteuzi mkali

Misheni hizi ni za kawaida kwa Morocco, ambayo ina mamilioni ya wahamiaji katika nchi za Ulaya. Kila Ramadhani, wasomi mia kadhaa huvuka Mediterania ili kuandamana na Waislamu wa Morocco wanaotaka kufanya hivyo.

Mchakato wa uteuzi hata hivyo ni mkali sana, lakini kulingana na vyombo vya habari kadhaa vya Morocco, masharti ya kupita katika uteuzi huo ni wa kutokuwa na mke na watoto. Kulingana na Gazeti la kila siku la Assabah, wizara ya Habbous kwa hivyo imeamua kuweka masharti magumu ya maimamu kuteuliwa kuendesha ibada nje ya nchi hususan Ulaya. Ili kuepuka mshangao wowote mbaya mwaka ujao, itahitajika maimamu wawe na wake na watoto kabla ya kutumwa Ulaya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.