Pata taarifa kuu

Blinken atoa wito wa kuongezeka kwa uwekezaji wa Marekani nchini Nigeria

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken ameelezea matumaini yake siku ya Jumatano kwa ongezeko la vitega uchumi vya Marekani nchini Nigeria lakini akaomba nchi yenye uchumi mkubwa zaidi barani Afrika kuwahakikishia wawekezaji kuhusu uwezekano wa kurejesha fedha zao.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken akitoa hotuba wakati wa ufunguzi mkuu wa American Corner Lekki katika 21st Century Technologies mjini Lagos, Januari 24, 2024.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken akitoa hotuba wakati wa ufunguzi mkuu wa American Corner Lekki katika 21st Century Technologies mjini Lagos, Januari 24, 2024. © AFP
Matangazo ya kibiashara

 

Baada ya kukutana na Rais wa Nigeria Bola Tinubu siku ya Jumanne katika mji mkuu wa Abuja, alikwenda katika mji mkuu wa kiuchumi wa Lagos, mji mkuu wa zaidi ya wakazi milioni 20, kutembelea makampuni ya kompyuta na kuzindua nafasi mpya ya kutangaza teknolojia ya Marekani.

Amehakikisha kwamba Washington ina nia "katika kufanya kazi na Nigeria, katika kuwekeza nchini Nigeria, katika kuanzisha ushirikiano na Nigeria", nchi yenye idadi kubwa ya watu katika bara la Afrika. Lakini, ameongeza, "bado kuna changamoto za kusuluhishwa ili kuhakikisha kuwa hali ya biashara itapokelewa vema."

Ameongeza kuwa alizungumza na viongozi wa Nigeria kuhusu masuala kadhaa, "ikiwa ni pamoja na uwezekano wa kurejesha mitaji na changamoto inayoendelea ya kutokomeza rushwa." Kampuni za kigeni zinazofanya kazi nchini Nigeria lazima hakika zitafute kibali kutoka kwa benki kuu ili kurejesha fedha katika nchi yao.

Mashirika ya ndege ya kigeni yamelalamikia ucheleweshaji wa kufikia mamilioni ya dola ya faida zilizozuiwa, kulingana mashirika hayo ya ndege, nchini Nigeria. Akiba ya kigeni ya nchi hiyo kubwa barani Afrika imeshuka katika siku za hivi karibuni kutokana na kushuka kwa bei ya mafuta duniani lakini pia kushuka kwa uzalishaji wa kitaifa.

Bwana Blinken hatimaye amekaribisha "mageuzi ya kiuchumi ya ujasiri" ya rais mpya wa Nigeria, hata kama "kwa muda mfupi", yalikuwa "yalikuwa mabaya" kwa watu walio katika mazingira magumu zaidi.

Baada ya Nigeria, mshirika muhimu wa Marekani katika eneo ambalo nchi nyingi zaidi zinajitenga na nchi za Magharibi, kwa manufaa ya China au Urusi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani atazuru Angola katika sehemu ya ziara yake ya Afrika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.