Pata taarifa kuu
KATIBA-USALAMA

Katiba mpya nchini DRC? Kwa upande wa upinzani, Félix Tshisekedi amevuka Rubicon

Rais Félix Tshisekedi hajatangaza kupinga uwezekano wa marekebisho ya Katiba karibu miezi mitano baada ya uchaguzi mkuu na miaka minne tangu kumalizika kwa muhula wa pili na wa mwisho wa rais. Wakati wa ziara yake barani Ulaya iliyompeleka Ujerumani, Ufaransa na Ubelgiji kukutana na watoa maamuzi na wanadiaspora, rais wa DRC alitangaza kuundwa kwa tume ambayo inapaswa kutafakari juu ya Katiba mpya. Tangazo ambalo linatia wasiwasi upinzani na mashirika ya kiraia.

Félix Tshisekedi mjini Paris, mapema mwezi Mei 2024.
Félix Tshisekedi mjini Paris, mapema mwezi Mei 2024. AFP - LUDOVIC MARIN
Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu wa Kinshasa, Pascal Mulegwa

Alipoulizwa na wajumbe wa diaspora huko Brussels kuhusu uwezekano wa kubadilishwa kwa Katiba, Rais Félix Tshisekedi hakupinga hili na akatangaza kwamba anataka Katiba "inayostahili nchi yetu". Upinzani tayari una hofu kuwa rais anaweza kupunguza idadi ya mihula yake hadi sifuri.

Mbunge Christian Mwando, ambaye anaongoza kundi la wabunge wa upinzani katika Bunge la taifa, anaona ni “jaribio la kuwania muhula wa tatu na kwamba hatuwezi kukubali na hatutakubali. Huu ni ukosefu kamili wa uongozi. Tshisekedi lazima achukue majukumu yake kwa Jamhuri na sio kuwalaumu wengine kila wakati na sio kulaumu Katiba ya nchi. Katiba ya nchi iko wazi, Katiba ya nchi ni nzuri. Kwa upande wengi wanasema, alipaswa kuweka nchi katika mpangilio lakini hakufanya hivyo. Si lazima kumshtumu mtu yeyote au hata Katiba. "

Jean-Claude Katende kutoka shirika la Kutetea Haki za Binadamu (ASADHO), anabaini kwamba kwa tangazo hili rais amevuka Rubicon (kuchukua uamuzi usiorejelewa). “Hata kwa muungano mtakatifu, kuna wengi ambao hawatakubali kwamba idadi ya mihula ibadilishwe, muda wa mamlaka na mbinu ya kuteuliwa kwa rais kubadilika. Kufungua mlango huu kungempa uhalali mtu yeyote anayetumia njia hata zisizo halali kutetea Katiba.

Tangu kuapishwa kwake mwezi Januari mwaka huu kwa muhula wake wa pili, Rais Félix Tshisekedi ameendelea kushtumu Katiba kwa kucheleweshwa kwa uanzishwaji wa taasisi za kisiasa. Ofisi ya Bunge imeshindwa kuwekwa, Waziri Mkuu aliyeteuliwa mwezi mmoja uliopita bado hajatangaza wazi serikali yake, ambayo uundaji wake unategemea zaidi maamuzi ya rais.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.