Pata taarifa kuu

Wanawake 35 waliokuwa wakirejea kutoka kwenye harusi watekwa nyara kaskazini mwa Nigeria

Takriban wanawake thelathini na watano waliokuwa wakirejea kutoka kwenye harusi walitekwa nyara na watu wenye silaha katika jimbo la Katsina kaskazini-magharibi mwa Nigeria, vyanzo vya polisi vimeliambia shirika la habari la AFP. Utekaji nyara huu wa watu wengi ndio mkubwa zaidi katika msururu wa utekaji nyara wa hivi majuzi unaoathiri nchi nzima.

Utekaji nyara ili kulipwa fidia ni tatizo kubwa nchini Nigeria, ambapo magenge yanaendesha shughuli zao kwenye barabara kuu, katika nyumba za waathiriwa na hata shuleni.
Utekaji nyara ili kulipwa fidia ni tatizo kubwa nchini Nigeria, ambapo magenge yanaendesha shughuli zao kwenye barabara kuu, katika nyumba za waathiriwa na hata shuleni. © AFP
Matangazo ya kibiashara

 

"Watu wanaoshukiwa kuwa majambazi wenye silaha wamewavizia na kuwateka nyara wanawake 35" waliokuwa wakirejea kutoka kwenye harusi eneo la Sabuwa, usiku wa Alhamisi kuamkia Ijumaa, amesema msemaji wa polisi, Abubakar Aliyu.

Nasiru Muaz, Kamishna wa Usalama wa Ndani wa Jimbo la Katsina, amesema idadi ya watu waliotekwa nyara wakati wakimsindikiza bibi harusi nyumbani kwake inaweza kuwa kubwa zaidi.

"Maafisa walikwenda kijijini na kujua kwamba watu 53 walitekwa nyara," Muaz amesema. "Ilikuwa hatari sana kwa msafara uliombeba bibi harusi kuendesha gari gizani katika eneo ambalo majambazi hufanya mashambulizi ya mara kwa mara. Majambazi walichukua fursa hii na kuwateka nyara," ameongeza.

"Hii ndiyo sababu tunatoa tahadhari ya wakazi wa wilaya nane zilizojaa majambazi (Sabuwar, Dandume, Faskari, Kankara, Safana, Da muss, Batsari na Jibia) kwa haja ya kuepuka kusafiri usiku," ameongeza Kamishna wa Usalama wa Ndani katika Jimbo la Katsina.

Operesheni ya polisi kuwatafuta mateka hao inaendelea, polisi imesema. Utekaji nyara ili kulipwa fidia ni tatizo kubwa nchini Nigeria, ambapo magenge yanaendesha shughuli zao kwenye barabara kuu, katika nyumba za waathiriwa na hata shuleni. Wanaendesha ukatili wao huo kutoka kambi zinazopatikana katika misitu ya kaskazini-magharibi na majimbo ya kati.

Mapema mwezi wa Januari, watu wenye silaha waliwateka nyara watawa watano karibu na mji mkuu, Abuja, na kumuua mmoja wao wakati tarehe ya mwisho ya malipo ya fidia ilipoisha, na hivyo kuzua taharuki nchi nzima. Wiki iliyopita, viongozi wawaili wa kijadi waliuawa katika shambulizi katika jimbo hilo, huku watu wenye silaha wakimpiga risasi kiongozi wa kimila na kumteka nyara mke wake katika Jimbo la Kwara.

Rais wa Nigeria Bola Ahmed Tinubu aliingia madarakani mwaka 2023 na kuahidi kukabiliana na ukosefu wa usalama nchini humo, ikiwa ni pamoja na makundi ya wanajihadi, majambazi Kaskazini-mashariki pamoja na kuongezeka kwa ghasia za kikabila katika majimbo ya Kati. Kampuniinayotoa nasaha kwa usimamizi wa majanga nchini Nigeria, SBM Intelligence, imesema kuwa imerekodi watu 3,964 waliotekwa nyara nchini Nigeria tangu kuanza kwa muhula wa Bola Ahmed Tinubu mwezi Mei 2023.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.