Pata taarifa kuu

Gambia: Mashirika mbalimbali yapinga mswada unaolenga kuhalalisha ukeketaji

Nchini Gambia, ambako ukeketaji umepigwa marufuku tangu mwaka 2015, mbunge aliwasilisha mswada mwanzoni mwa mwezi Machi ili kufanya kitendo hiki kuwa halali tena. Muungano wa Wanawake wa Kiafrika dhidi ya ukataji na unyanyasaji unaohusishwa na mila uliandaa maandamano siku ya Alhamisi, Mei 2, mjini Dakar kukataa mradi huu.

Mwanamke akiwa mbele ya bango la kutaka kukomeshwa kwa ukeketaji (picha ya kielelezo).
Mwanamke akiwa mbele ya bango la kutaka kukomeshwa kwa ukeketaji (picha ya kielelezo). AFP - KAMBOU SIA
Matangazo ya kibiashara

Pendekezo hili lililowasilishwa na mbunge nchini Gambia limekataliwa vikali na vyama vingi, haswa muungano wa mashirika unaopinga ukeketaji.

Akihojiwa na RFI, Mame Sira Konaté, katibu mkuu wa muungano huo anatoa wito wa "kukaa mbele ya Bunge la Gambia dhidi ya maamuzi ya uhalifu dhidi ya wasichana wetu."

"Ni hisia ya hofu ambayo inatuingia kwa sababu tunajiambia kwamba, ikiwa tutaanza kupoteza mafanikio ambayo mama zetu walipigania kwa miaka kadhaa, inakuwa hatari sana kwetu. "

"Tunatoa wito kwa watu wote kutetea haki za wanawake"

"Pia ina maana ya kusema hapana, kupitia hatua zilizochukuliwa, kwa kufutwa kwa sheria dhidi ya ukeketaji nchini Gambia. Inamaanisha pia kuzindua kampeni ya uhamasishaji na kuandaa msafara wa kwenda Gambia na, ikiwa ni lazima, kufanya kikao.

"Lakini jambo la kwanza ambalo tungependa kufanya litakuwa kumshawishi Rais wa Jamhuri ya Gambia, Bw. Barrow, aondoe mswada huu kwa sababu katika Bunge la ambia ambapo kuna wanawake wanne tu, ni wazi, tunafahamu ukweli kwamba ikiwa mswada huu utapigiwa kura, basi utapitishwa.

"Pia tunaifikiria Senegal. Gambia inapakana na Senegal na familia za Senegal zinaweza kwenda Gambia na kuwakeketa binti zao. Tunatoa wito kwa watu wote kutetea haki za wanawake, kwa miundo yote inayopigana dhidi ya ukatili dhidi ya wanawake na wasichana. "

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.