Pata taarifa kuu

Nigeria: Rais Tinubu amemsimisha kazi waziri anayehusika na masuala ya binadamu

Nairobi – Rais wa Nigeria Bola Tinubu amemsimisha kazi, Betta Edu Waziri anayehusika na masuala ya binadamu na kupambana na umasikini.

Rais Tinubu amesema, Waziri huyo amesimamishwa kazi baada ya kutumia Benki binafsi kuhifadhi fedha za maendeleo kwenye Wizara yake
Rais Tinubu amesema, Waziri huyo amesimamishwa kazi baada ya kutumia Benki binafsi kuhifadhi fedha za maendeleo kwenye Wizara yake AP - Lewis Joly
Matangazo ya kibiashara

Kupitia kwa msemaji wake Ajuri Ngelale, rais Tinubu amesema, Waziri huyo amesimamishwa kazi baada ya kutumia Benki binafsi kuhifadhi fedha za maendeleo kwenye Wizara yake.

Ngelale, ameongeza kuwa hatua hii imekuja baada ya kufanyika uchunguzi na taasisi ya kupambana na rushwa, kwenye Wizara mbalimbali za serikali kuhusu matumizi ya fedha za umma.

Edu amesimamishwa kazi baada ya vyombo vya Habari nchini Nigeria, kuripoti kuwa, aliagiza kupelekwa kwa Naira Milioni 585 zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya watu masikini, kuhifadhiwa kwenye akaunti binafsi.

Baada ya kuingia madarakani mwaka uliopita, rais Tinubu aliahidi kupambana na rushwa, na mwezi mmoja tu baada ya kuchukua madaraka, alimsimamisha kazi mkuu wa Tume inayopambana na uhalifu wa kifedha kwa matumizi mabaya ya ofisi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.