rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Ufaransa Iran

Imechapishwa • Imehaririwa

Mtafiti wa Ufaransa Roland Marchal azuiliwa nchini Iran tangu msimu wa joto

media
Rais wa Jamuhuri ya Kiislamu ya Iran, Hassan Rohani, na Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi Ali Khamenei, mwaka 2017 Tehran. HO / KHAMENEI.IR / AFP

Vyombo kadhaa vya habari vimeripoti Jumatano hii, Oktoba 16, 2019 kwamba mtafiti wa pili, raia wa Ufaransa, anashikiliwa nchini Iran tangu mwezi Juni mwaka huu.


RFI ina vithibitisho vya kukamatwa Roland Marchal, mtaalam wa Afrika, aliyekamatwa jijini Tehran wakati mmoja na mtaalam mwengine, raia wa Ufaransa mwenye asili ya Iran Fariba Adelkhah.

Roland Marchal ni mtafiti katika shirika lisilo la kiserikali la CNRS-CERI, hususan nchini Sudani. Alikamatwa na kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi kwenye uwanja wa ndege wa Tehran wakati alipokuwa akishuka kutoka ndani ya ndege mwanzoni mwa mwezi Juni. Fariba Adelkhah, ambaye alikuwa kwenye uwanja huo wa ndege, alikamatwa na kufungwa jela wakati huo huo.

Ufaransa imeamua kusalia kimya na kujizuia kuzungumza chochote kwa umma kuhusu kuzuiliwa kwa watafiti hao wawili, kwa kukataa kuweka hatarini mchakato unaoendelea wa kutaka waachiliwe huru.

Lakini mwezi Julai, wakati vyombo vya habari vya Iran vilipoweka wazi taarifa hii ya kuzuiliwa Fariba Adelkhah, anayeshutumiwa kosa la uhaini na kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi, Paris hatimaye imeomba hadharani aachiliwe huru.

Mamlaka nchini Ufaransa hijazungumzia chochote mpaka sasa kuhusu taarifa ya kuzuiliwa kwa Roland Marchal.