Pata taarifa kuu

Nagorno-Karabakh: Urusi yatangaza kuanza kuwaondoa wanajeshi wake wa kulinda amani

Wanajeshi wa Urusi waliotumwa Nagorno-Karabakh tangu msimu wa joto mwaka 2020 wameanza kuondoka katika eneo la Nagorno-Karabakh, Kremlin imetangaza siku ya Jumatano, Aprili 17, miezi saba baada ya Azerbaijan kuchukua tena eneo hili lililodhibitiwa kwa miongo mitatu na waasi wa Armenia.

Askari wa Urusi wakihusika katika ulinzi wa amani huko Nagorno-Karabakh. Hapa, ilikuwa tarehe 10 Novemba 2020.
Askari wa Urusi wakihusika katika ulinzi wa amani huko Nagorno-Karabakh. Hapa, ilikuwa tarehe 10 Novemba 2020. REUTERS/Francesco Brembati
Matangazo ya kibiashara

"Ndiyo, ndivyo hivyo," msemaji wa rais wa Urusi Dmitry Peskov amewaambia waandishi wa habari, akithibitisha ripoti za vyombo vya habari vya Azerbaijan. Hikmet Hajiev, mshauri wa Rais wa Azerbaijan Ilham Aliyev, amesema uamuzi wa kujiondoa umechukuliwa katika ngazi ya "juu" kati ya Baku na Moscow.

“Mchakato umeanza. Wizara za Ulinzi za Azerbaijan na Urusi zinafanya shughuli zinazohitajika kutekeleza uamuzi huu,” amesema, akinukuliwa na shirika la habari la serikali la Azertag.

Ujumbe wa kulinda amani wa kutekeleza usitishaji mapigano

Mnamo msimu wa joto wa mwaka 2020, vita vya wiki sita viligonga Azerbaijan na waasi wanaoungwa mkono na Armenia kudhibiti eneo la Nagorno-Karabakh, na kusababisha vifo vya watu 6,500. Vita hivi vilimalizika kwa kushindwa kwa nguvu kwa vikosi vya Armenia, ambavyo vililazimika kuacha maeneo muhimu. Kisha Urusi ilituma kikosi cha kulinda amani cha wanajeshi 2,000 kutekeleza masharti ya kusitisha mapigano na kuwaondoa wanajeshi wanaotaka kujitenga.

Mnamo mwezi wa Septemba 2023, Azerbaijan iliongoza shambulio jipya la kubwa na kudhibiti eneo la Nagorno-Karabakh , bila vikosi vya Urusi kuingilia kati, na kumaliza miongo mitatu ya mzozo kwa udhibiti wa eneo hilo. Kisha Armenia ilishutumu vikali kutochukua hatua kwa mshirika wake, Urusi, ambaye kwa muda mrefu alichukuliwa kuwa msuluhishi wa jadi katika Caucasus, na tangu wakati huo imejisogeza kwa nchi Magharibi.

Mazungumzo yanashindwa kusonga mbele

Marekani, Umoja wa Ulaya na Urusi zimejaribu kupatanisha kutiwa saini kwa mkataba wa amani wa kutatua mizozo ya eneo hilo kati ya Baku na Yerevan, lakini mazungumzo hayo yameshindwa kuzaa matunda. Baku inadai vijiji vinane vinavyoshikiliwa na Armenia na inadai kuundwa kwa ukanda wa ardhi kupitia eneo la Armenia la Siounik - kusini - ili kuunganisha Azerbaijan na eneo lake la Nakhchivan, kisha na Uturuki, mshirika wake.

Kwa upande wake, Yerevan inadai eneo laa Artsvashen - Bashkend huko Azeri -, iliyoko katika eneo la Azerbaijan na kudhibitiwa na Baku tangu miaka ya 1990, pamoja na maeneo yaliyotekwa na Azerbaijan kwa miaka mitatu iliyopita na ambayo iko ndani ya mipaka ya Armenia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.