Pata taarifa kuu
UN-MAREKANi-IRAN-USALAMA

Trump atishia kuongeza shinikizo zaidi kwa Iran

Rais wa Marekani Donald Trump, katika mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa mjini New York, ametishia kuongeza shinikizo zaidi kwa Iran, wakati nchi za Ulaya zinaendelea kuaongeza juhudi kujaribu kupunguza mvutano kati ya mataifa hayo mawili.

Donald Trump kwenye Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Septemba 24, 2019.
Donald Trump kwenye Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Septemba 24, 2019. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Katika hotuba iliyosomwa kwa sauti isiyo ya kawaida, bila shauku au wakati mgumu, Donald Trump, ambaye ameonekana amechoka, ameongeza onyo kali dhidi ya Tehran.

"Wakati mwenendo wa vitisho wa Iran utaendelea, vikwazo havitaondolewa, bali vitaongezwa ," Trump amesema mbele ya wawakilishi wa nchi wanachama 193 wa Umoja wa Mataifa waliokusanyika kwa Mkutano wao Mkuu wa kila mwaka.

"Nchi zote zina jukumu la kuchukua hatua, hakuna serikali inayowajibika ambayo inapaswa kuunga mkono damu kumwagika nchini Iran," amesema Trump, bila hata hivyo kuweka mbele mapendekezo mapya na kutumia tena kauli aliyotoa katika hotuba zake miaka miwili iliyopita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.