Pata taarifa kuu
UFARANSA-IRAN-MAREKANI-USALAMA

Macron atoa wito kwa Iran na Marekani kusitisha mvutano

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amezitaka Iran na Marekani kuketi kwenye meza ya mazungumzo ili kutatua mzozo unaoendelea kati ya nchi hizo mbili.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akizungumza kuhusu jindsi ya kulinda msitu wa Amazon katika Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa, New York, Septemba 23, 2019.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akizungumza kuhusu jindsi ya kulinda msitu wa Amazon katika Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa, New York, Septemba 23, 2019. REUTERS/Lucas Jackson
Matangazo ya kibiashara

Wakati mvutano ukiendelea kutokota baina ya Marekani na Iran hasa kuhusu tuhuma za moja kwa moja kuhusika Teheran kuhusika na mashambulizi ya hivi karibuni ya miundombinu ya visima vya mafuta kwa mshirika mkuu wa Marekani Saudia Arabia, Ufaransa inasema kwanza inalaani mashambulizi hayo, lakini pia yatoa wito kwa pande zote kuzuia kutoka kwa hali mbaya zaidi.

Akizungumza na waandishi wa habari Jumatatu wiki hii, kando na mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya tabia nchi, rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amesema anakutana na pande zote ili kujaribu kupunguza joto lililopo.

Mashambulizi ya hivi karibuni yaliodaiwa kuvurumishwa na waasi wa kundi la kishia wa Houthi katika miundo mbinu ya mafuta ya Saudia Arabia yamezua mzozo mpya baina ya Iran na Marekani pamoja na washirika wake ambapo hawaamini kwamba waasi hao wa Houthi wanaoungwa mkono na Iran wana uwezo wa kumiliki makombora yaliotumiwa.

Rais wa Ufaransa, pia alimwambia Rais Rohani kwamba njia ya kuondokana na mvutano ipo. "Wakati umefika kwa Iran kutumia nafasi hiyo, amebaini Emmanuel Macron. Lakini washirika wa karibu wa rais wa Ufaransa, hawana imani kabisa na uwezekano wa kufanyika kwa mkutano mjini New York kati ya Rais Donald Trump na Hassan Rohani, unaopendekezwa na Paris.

Rais wa Marekani alimjibu Emmanuel Macron, akisema hahitaji mpatanishi na kwamba kwa sasa, hakuna mkutano wowote uliopo kwenye ajenda, hata ikiwa mlango haujafungwa kabisa.

Rais Macron ataendeleza juhudi zake za upatanishi hadi kuondoka kwake nchini Marekani Jumanne hii usiku.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.